Mrisho Ngass

image

amefunga mabao matatu leo katika ushindi wa 5-2 wa Yanga dhidi wenyeji Komorozine mjini Moroni katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika. Mabao mengine ya Yanga yamefungwa nna Hamisi Kiiza kulia na Simon Msuva na sasa timu hiyo ya Dar es Salaam inafuzu kwa ushindi wa jumla wa 12-2 baada ya awali kushinda 7-0, Ngassa akifunga hat trick pia na itamenyana na mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri katika Raundi ya Kwanza mwezi ujao.

image

Advertisements

Simba vs mbeya city

image

SIMBA SC imegawana pointi na wenyeji Mbeya City baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 Uwanja wa Sokoine Mbeya.Matokeo hayo yanaifanya Mbeya itimize pointi 35 sawa na Yanga SC iliyo nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao wakati Simba inatimiza pointi 32 na inabaki nafasi ya nne. Hadi mapumziko, tayari Mbeya City walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na Deogratius Julius kwa penalti dakika ya 13, akimchambua vizuri kipa Mghana, Yaw Berko.Wachezaji wa Mbeya City wakishangilia bao la kuongoza kabla ya Simba kusawazisha leo Uwanja wa SokoinePenalti hiyo ilitolewa kufuatia beki Joseph Owino kuunawa mpira katika harakati za kuokoa krosi ya Deus Kaseke kutoka wingi ya kushoto.Mbeya City walitawala mchezo na kipindi cha kwanza na Simba SC ilimtumia Ramadhani Singano ‘Messi’ kushambulia, ambaye hata hivyo aliwekewa ulinzi mkali na mabeki wa timu ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya.Mshambuliaji Mrundi Amisi Tambwe aliunganishia juu ya lango kwa kichwa mipira miwili ya adhabu iliyopigwa na Amri Kiemba kipindi cha kwanza, kufuatia Messi kuangushwa. Kipa wa Simba SC, Yaw Berko akiwa amepiga magoti baada ya kufungwa kwa penalti leo Uwanja wa SokoineKocha Mkuu wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic kwa pamoja na wasaidizi wake Suleiman Matola na Iddi Pazi waliwafuata marefa katikati ua Uwanja kuwalalamikia walikuwa wanawapendelea wenyeji na kuwaomba kipindi cha pili wachezeshe haki. Ramadhani Singano ‘Messi’ wa Simba SC akiwatoka mabeki wa Mbeya City leoKipindi cha pili, Simba SC ilibadilika mno na kuongeza kasi ya mashambulizi, hatimaye kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 mfungaji Mrundi Amisi Tambwe, aliyemalizia krosi ya Haroun Chanongo.Baada ya Simba SC kusawazisha, kasi ya mchezo iliongezeka kwa pande zote mbili, timu zote zikishambuliana kwa zamu.Kikosi cha Mbeya City kilikuwa; David Burhan, John Kabanda, Hamad Kibopile/Mwagane Yeya dk31, Deo Julius, Yussuph Abdallah, Anthony Matogolo, Peter Mapunda, Steven Mazanda, Paul Nonga/Francis Castor dk81, Hassan Mwasapili na Deus Kaseke. Simba SC; Yaw Berko, William Lucian ‘Gallas’, Henry Joseph, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Ramadhani Singano ‘Messi’/Awadh Juma dk66, Said Ndemla/Christopher Edward dk76 , Amisi Tambwe, Amri Kiemba na Haroun Chanongo/Zahor Pazi dk54.Katika mechi nyingine za leo, Rhino Rangers imetoka sare ya 1-1 na Mgambo JKT Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora, bao la wenyeji likifungwa na Gideon Brown dakika ya 30 na wageni wakisawazisha dakika ya 52 kupitia kwa Ally Bolly.Ashanti United imetoka sare ya bila kufungana na Kagera Sugar Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam na bao pekee la Peter Michael dakika ya 49 limetosha kuwapa Prisons ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.JKT Oljoro imetoka sare ya bila kufungana na JKT Ruvu Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, wakati bao pekee la Said Dilunga dakika ya 85 limeipa Ruvu Shooting ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.

Kila la kheri Azam fc

image

AZAM FC imefika salama mjini Beira, Msumbiji tayari kwa mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Ferroviario de Beira Jumapili mjini humo.Msafara wa Azam ulioondoka bila kocha wake Msaidizi, Kalimangonga Sam Daniel Ongala ‘Kali Ongala’ ulifika jana na leo umeanza mazoezi kwenye Uwanja wa wenyeji wao hao.Mfungaji wa bao pekee la Azam Chamazi dhidi ya Feroviario, Kipre Herman Tchetche akiwa amejibanza kukwepa mvua inayoendelea mjini BeiraKatibu wa Azam FC, Nassor Idrisa ‘Father’ ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kutoka Beira kwamba timu imefikia katika hoteli ya Rainbow na mechi itachezwa Jumapili Saa 8:00 mchana kwa saa za Msumbiji na saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.Father amesema mchezo huo utaonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Azam TV. “Lakini mvua kubwa inanyesha huku, inanyesha kutwa nzima, ila maandalizi ni mazuri na tumekuja na viatu vya kuchezea kwenye mvua, hivyo tupo kamili,”alisema Father.Azam FC iliyoanza kwa ushindi mwembamba wa 1-0 Jumapili Uwanja wa Azam Complex Jumapili, iliondoka jana asubuhi Dar es Salaam kwa ndege ya Fast Jet hadi Johannesburg, Afrika Kusini ambako waliunganisha ndege ya shirika la Msumbiji kwenda Beira.Uwanja wa FerroviarioMvua kutwa nzimaWachezaji wakiwa uwanjani tayari kwa mazoeziAzam imeondoka na wachezaji 21 ambao ni makipa; Mwadini Ali, Aishi Manula na Jackson Wandwi, mabeki Luckson Kakolaki, Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Aggrey Morris, Said Mourad, David Mwantika, viungo Ibrahim Mwaipopo, Kipre Balou, Jabir Aziz, Salum Abubakar, Himid Mao, Khamis Mcha na washambuliaji John Bocco, Kipre Tchetche, Brian Umony, Seif Abdallah, Gaudence Mwaikimba na Ismael Kone.Benchi la Ufundi linaongozwa na Kocha Mkuu Mcameroon, Joseph Marius Omog, kocha wa makipa Iddi Abubakar, Meneja Jemadari Said, Daktari Mkuu Mwanandi Mwankemwa, Mchua misuli Paul Gomez na mtunza vifaa Yussuf Nzawila. Azam inahitaji sare yoyote baada ya ushindi wa 1-0 nyumbani ili kusonga mbele.

Yanga inauwezo yakuitoa misri

image

KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Sekilojo Johnson Chambua amesema kwamba Yanga SC inaweza kuitoa Al Ahly katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kwa kuwa soka ya Misri hivi sasa imeshuka tofauti na miaka ya nyuma enzi zao wanacheza, lakini wanatakiwa kufanyia kazi mambo matatu.Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo mchana, Chambua amesema kwamba Yanga ina matatizo matatu, kwanza hawamudu kucheza dakika 90 kwa kasi ile ile, pili safu ya ulinzi inakatika na safu ya ushambuliaji haina makali ya kutosha, mambo ambayo kama watayafanyia masahihisho, wanaweza kuweka historia kwa kuwa timu ya kwanza ya Tanzania kuitoa mashindanoni Ahly.Magwiji; Sekilojo Chambua kulia akiwa na Edibily Lunyamila enzi zao miaka ya 1990“Mara ya mwisho nimeiona Yanga inacheza na Mbeya City pale Uwanja wa Taifa, wakashinda bao 1-0. Niseme tu Yanga ilicheza vizuri, lakini washambuliaji wake walikosa mabao mengi kutokana na kukosa ubunifu wanapofika kwenye eneo la wapinzani,”alisema kiungo huyo wa zamani wa Tukuyu Stars ya Mbeya na Yanga SC ya Dar es Salaam.Chambua alisema mchezaji David Luhende anayetumika kama winga wa kushoto kwa sasa pamoja na Simon Msuva anayecheza kulia, walikuwa wanapata mipira ya kuingia nayo kwenye boksi, lakini wakawa ama wanatia krosi au wanarudi nyuma. “Hawakutakiwa kufanya vile, walitakiwa kufanya kama ambavyo Edi (Edibily Lunyamila) alikuwa anafanya wakati ule tunacheza naye, alikuwa anaingia ndani. Kitendo cha kupiga krosi tu kinawapa nafasi hata mabeki kuokoa, lakini kama wangekuwa wanaingia ndani wangeweza kufunga au kutengeneza nafasi za wengine kufunga,”.  Chambua alisema kwamba iwapo mawinga hao wa Yanga watabadilika na kuingia na mpira kwenye eneo la hatari la wapinzani, kasi ya mashambulizi ya Yanga itaongezeka na hiyo inaweza kuzalisha mabao mengi.Lakini Chambua alimpongeza mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa anavyocheza hivi sasa, kwamba anakosa tu mtu wa kushirikiana naye pale mbele, ila makocha wa Yanga kama watampatia ‘pacha’ mzuri mchezaji huyo, safu ya ushambuliaji ya timu hiyo itakuwa hatari zaidi.Kuhusu safu ya ulinzi, Chambua alisema kwamba mtu mmoja tu anacheza vizuri kwa sasa, ambaye ni beki wa kushoto, Oscar Joshua lakini wengine haswa mabeki wa kati wanatakiwa sana kurekebisha uchezaji wao.“Mabeki wa kati wa Yanga wanakatika sana, sasa ile ni hatari mno unapokutana na timu kama Ahly yenye uwezo mkubwa wa fikra, mbinu na ufundi. Kwa kweli, Yanga lazima wabadilishe staili ya uchezaji wao kama kweli wanataka kuitoa Ahly, hili  ni jambo ambalo makocha wanatakiwa kulifanyia kazi mapema sana,”alisema.Chambua pia aliisifu Mbeya City na kusema kwamba hiyo Tukuyu Stars mpya mkoani humo, lakini akawashauri waboreshe mbinu za kiufundi.“Siku wanacheza na Yanga, wachezaji wa Yanga walikuwa wanafanya makosa mengi sana ambayo kama Mbeya City ingekuwa vizuri sana kiufundi, ingeyatumia kusawazisha na hata kuongeza bao,”alisema.Yanga SC inaweza kukutana na Al Ahly mwezi ujao katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, iwapo itamalizia vyema Raundi ya Awali mwishoni mwa wiki hii, baada ya Jumamosi kuitandika mabao 7-0 Komorozine ya Comoro katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba yaanza vibaya 1-0

image

SIMBA SC imelala bao 1-0 jioni ya leo mbele ya Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.Kwa mara nyingine leo kipa Ivo Mapunda amefungwa bao rahisi, baada ya kumtemea mpira mshambuliaji Fully Maganga dakika ya 29 kufuatia mpira wa adhabu.Wachezaji wa Simba SC walipambana sana kujaribu kusawazisha bao hilo tangu hapo, lakini Mgambo Shooting leo walisimama imara kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.Kwa matokeo hayo, Simba SC inabaki na pointi zake 31 baada ya kucheza mechi 17, wakati Mgambo inatimiza pointi 12 na inaendelea kushika mkia.Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dk57, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Awadh Juma/Uhuru Suleiman dk62, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amisi Tambwe na Ali Badru/Haroun Chanongo dk46.Mgambo Shooting; Saleh Tendega, Bashir Chanache, Salim Kipaga, Bakari Mtama, Novaty Lufunga, Mohamed Samatta, Peter Mwalyanzi, Bolly Ajali, Fully Maganga Malima Busungu.

YANGA 7 VS COMORRO O

image

mmoja Raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kufuatia ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Komorozine ya Comoro jioni hii katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali, Ligi ya Mabingwa Afrika.Washambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa alifunga mabao matatu, Mrundi Didier Kavumbangu mawili, Mganda Hamisi Kiiza moja na lingine beki Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’.Kwa ushindi huo, Yanga sasa inahitaji sare au kufungwa si zaidi ya mabao 6-0 katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo ugenini ili kusonga mbele, ambako itakutana na Al Ahly ya Misri.Wauaji; Mrisho Ngassa kushoto akiwapungia mikono mashabiki baada ya kukamilisha hat trick katika ushindi wa 7-0 wa Yanga dhidi ya Komorozine jioni hii Uwanja wa Taifa. Wengine kulia kwake ni SImon Msuva na Didier Kavumbangu aliyefunga mabao mawiliKatika mchezo huo uliochezeshwa na refa Hassan Mohamed Hagi, aliyesaidiwa na Hamza Hagi Abdi na Bashir Abdi Suleiman wote kutoka Somalia, hadi mapumziko tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0.Mabao hayo yalifungwa na Ngassa dakika ya 14 na Cannavaro dakika ya 20, wote wakitikisa nyavu kwa kichwa baada ya mipira kutoka pembeni.Ngassa alifunga akimalizia krosi maridadi ya Simon Msuva kutoka wingi ya kulia, wakati Cannavaro aliunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na David Luhende kutoka wingi ya kulia, kufuatia Mbuyu Twite kuchezewa rafu.Mahambuliaji Mganda Hamisi Friday Kiiza aliikosesha Yanga SC mabao zaidi ya manne kipindi cha kwanza kwa kushindwa kuepuka mitego ya kuotea aliyokuwa akiwekewa na mabeki wa Komorozine.Mrisho Ngassa alikuwa mwiba leoYanga ilitawala mchezo kipindi chote cha kwanza na kufanya mashambulizi mengi, lakini pamoja na kupata mabao mawili walitengeneza nafasi zaidi ya nane walizoshindwa kuzitumia.   Kipindi cha pili, Yanga ilianza na mabadiliko, ikimpumzisha David Luhende na kumuingiza Kavumbangu ambaye alikwenda kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji hadi mabao matano zaidi yakapatikana.Kavumbangu mwenyewe alianza dakika ya 57 akimalizia pasi ya Haruna Niyonzima, akafuatia Kiiza dakika ya 59 akimalizia pasi ya Kavumbangu, Ngassa mara mbili mfululizo dakika ya 64 na 68 na Kavumbangu akahitimisha karamu ya mabao dakika ya 80.Kikosi cha Yanga kilikuwa; Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan/Rajab Zahir dk76, Frank Domayo, Simon Msuva/Hassan Dilunga dk71, Haruna Niyonzima, Hamisi Kiiza, Mrisho Ngassa na David Luhende/Didier Kavumbangu dk46.Komorozine; Attoumani Farid, Ali Mohamed Mouhousoune, Nizar Amir, Abdou Moussoidi Kou, Ahamadi Houmadi Ali, Moidjie Ali, Mourthadhoi Fayssol, Attoumane Omar, Mohamed Erfeda/Imroina Ismael dk30, Mouyade Almansour Nafouondi na Ahmed Waladi Mouhamdi/Ghaidane Mahmoud dk80.