TANZANIA 0-ZIMBABWE 0

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imelazimishwa sare ya bila kufungana na Zimbabwe jioni hii katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hata hivyo, Zimbabwe wangeondoka na sherehe Uwanja wa Taifa, kama si Refa Ronnie Kalema aliyesaidiwa na Samuel Kayondo na Lee Okelo wote kutoka Uganda kuwakatalia bao zuri lililofungwa na Sithole Simba dakika ya 90.

Krosi nzuri ya Kapombe, Ulimwengu alishindwa kuunganisha nyavuni na kuikosesha Stars bao la wazi

Kwa ujumla, Tanzania haikuwafurahisha mashabiki wake leo pamoja na kuwa na kikosi chake kamili, wakiwemo washambuliaji tegemeo Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu wanaocheza TP Mazembe ya DRC, kiungo Mwinyi Kazimoto anayechezea Al Markhiya ya Qatar na beki Shomari Kapombe anayechezea AS Cannesd ya Ufaransa.
Stars iliuanza vyema mchezo huo, safu ya kiungo ikiundwa na chipukizi Hassan Dilunga aliyecheza pamoja na Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto.
Viungo hao waliweza kuwachezesha vizuri washambuliaji watatu wa Stars, Mrisho Ngassa, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta, lakini wakashindwa kutumia nafasi hizo vizuri kipindi cha kwanza.
Zimbabwe walizinduka baada ya dakika 10 na kucheza vizuri, wakitengeneza nafasi pia ambazo walishindwa kuzitumia.

Ivo Mapunda akiokota mpira nyavuni baada ya ZImbabwe kufunga bao lililokataliwa na refa

Safu ya kiungo ya Stars ilikufa ndani ya dakika 30 na Zimbabwe wakaanza kutawala mchezo. Kipindi cha pili, Kim alifanya mabadiliko ya viungo akiwaingiza Amri Kiemba na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kuchukua nafasi za Kazimoto na Dilunga na kidogo Stars ilianza kutawala sehemu ya katikati ya Uwanja, lakini iliishia kukosa mabao ya wazi.
Nafasi ambayo Stars wataijutia zaidi ni ya dakika ya 75, kufuatia Kapombe kutia krosi nzuri baada tya kupokea pasi ya Sure Boy, lakini Ulimwengu akazidiwa na kipa Tapiwa Kapini aliyedaka mpira miguuni mwake.
Kipa Ivo Mapunda alifanya kazi nzuri kwa kuokoa michomo mitatu ya hatari hali ambayo ilifanya ashangiliwe baada ya mechi.
Mashabiki walimzomea kocha Mdenmark Kim Poulsen baada ya mechi wakimuambia timu imemshinda na kumtaka aondoke.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ivo Mapunda, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/Himid Mao dk56, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Hassan Dilunga/Salum Abubakar dk51, Mwinyi Kazimoto/Amri Kiemba dk51, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Farid Mussa dk80.
Zimbabwe; Tapiwa Kapini, Ocean Mushere, Carrington Nyandemba, Obey Mureneheri/Misheck Mborai dk46, Themba Ndhlovu/Felix Chidungwe, Isaac Majari/Patson Jaure, Kapinda Wonder, Kundawashe Mahachi, Warren Dube/Nkosana Siwela, Lot Chiungwa/Gerald Ndhlovu na Simba Sithole.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s