TANZANITE SASA NI KALI SANA

TANZANITETIMU ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) imefuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla ya mabao 15-1 baada ya leo (Novemba 9 mwaka huu) kuibugiza Msumbiji mabao 5-1.
Kwa mujibu wa kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo mabao ya Tanzanite katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini Maputo yalipatikana kupitia kwa Sherida Boniface alipiga matatu (hat trick) wakati mengine yalifungwa na Vumilia Maarifa na Donesia Minja.

Msafara wa Tanzanite ulioongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho Jumapili (Novemba 10 mwaka huu) saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.

Tanzanite inayofundishwa na Rogasian Kaijage itacheza mechi ya raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini. Mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Desemba 6 na 8 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika Afrika Kusini kati ya Desemba 20-22 mwaka huu.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s