TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars imeanza taratibu

TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars imeanza taratibu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya kutoa sare ya 1-1 na mabingwa wa zamani wa Afrika, Zambia au Chipolopolo kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos, Kenya.
Katika mchezo huo wa Kundi B, Zambia ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ronald Kampamba dakika ya 41, akiunganisha kwa kichwa krosi ya Felix Katongo.
Zambia walitawala zaidi mchezo huo kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi zaidi ya nne za kufunga, lakini sifa zimuendee kipa Ivon Philip Mapunda aliyeokoa michomo kadhaa ya hatari.

 GOLI LA STARS
Mrisho Ngassa akishangilia baada ya Said Morad (hayupo pichani) kuisawazish Stars, huku kipa wa Zambia na mabeki wake wakiwa wameduwaa
Kipindi cha pili, Stars ilibadilika mno kiuchezaji, japokuwa wachezaji waliomaliza kipindi cha kwanza ndiyo wote waliorejea kuanza ngwe hiyo ya lala salama.
Kutokana na mshambulizi mfululizo langoni mwa Zambia, Bara walipata kona dakika ya 48 ambayo ilikwenda kuchongwa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na kuunganishwa nyavuni na Said Morad kwa kichwa.
Baada ya bao hilo, Zambia walianza kuutafuta mpira kwa tochi na kama si umahiri wa kipa wao, Nsabata Toaster kuokoa hatari nyingi, Stars wangeweza kuondoka na ushindi. 
Kwa matokeo hayo, Burundi inaongoza kundi hilo baada ya kuifunga Somalia 2-0 katika mchezo wa kwanza wa kundi hilo kwenye Uwanja huo.
Kikosi cha Stars kilikuwa; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk89, Hassan Dilunga/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk85, Elias Maguri/Haroun Chanongo dk72, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa.

 

Chipolopolo; Nsabata Toaster, Bronson Chama, Jimmy Chisenga/Kabaso Chongo dk67, Christopher Munthali, Rodrcik Kabwe, Stanley Nshimbi/Alex Nshimbi dk57, Sydney Kalume, Kondwani Mtonga, Felix Katongo/Salulani Phiri dk73, Ronald Kampamba na Festus Ndewe.  
Advertisements

TANZANIA 0-ZIMBABWE 0

TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imelazimishwa sare ya bila kufungana na Zimbabwe jioni hii katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hata hivyo, Zimbabwe wangeondoka na sherehe Uwanja wa Taifa, kama si Refa Ronnie Kalema aliyesaidiwa na Samuel Kayondo na Lee Okelo wote kutoka Uganda kuwakatalia bao zuri lililofungwa na Sithole Simba dakika ya 90.

Krosi nzuri ya Kapombe, Ulimwengu alishindwa kuunganisha nyavuni na kuikosesha Stars bao la wazi

Kwa ujumla, Tanzania haikuwafurahisha mashabiki wake leo pamoja na kuwa na kikosi chake kamili, wakiwemo washambuliaji tegemeo Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu wanaocheza TP Mazembe ya DRC, kiungo Mwinyi Kazimoto anayechezea Al Markhiya ya Qatar na beki Shomari Kapombe anayechezea AS Cannesd ya Ufaransa.
Stars iliuanza vyema mchezo huo, safu ya kiungo ikiundwa na chipukizi Hassan Dilunga aliyecheza pamoja na Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto.
Viungo hao waliweza kuwachezesha vizuri washambuliaji watatu wa Stars, Mrisho Ngassa, Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta, lakini wakashindwa kutumia nafasi hizo vizuri kipindi cha kwanza.
Zimbabwe walizinduka baada ya dakika 10 na kucheza vizuri, wakitengeneza nafasi pia ambazo walishindwa kuzitumia.

Ivo Mapunda akiokota mpira nyavuni baada ya ZImbabwe kufunga bao lililokataliwa na refa

Safu ya kiungo ya Stars ilikufa ndani ya dakika 30 na Zimbabwe wakaanza kutawala mchezo. Kipindi cha pili, Kim alifanya mabadiliko ya viungo akiwaingiza Amri Kiemba na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ kuchukua nafasi za Kazimoto na Dilunga na kidogo Stars ilianza kutawala sehemu ya katikati ya Uwanja, lakini iliishia kukosa mabao ya wazi.
Nafasi ambayo Stars wataijutia zaidi ni ya dakika ya 75, kufuatia Kapombe kutia krosi nzuri baada tya kupokea pasi ya Sure Boy, lakini Ulimwengu akazidiwa na kipa Tapiwa Kapini aliyedaka mpira miguuni mwake.
Kipa Ivo Mapunda alifanya kazi nzuri kwa kuokoa michomo mitatu ya hatari hali ambayo ilifanya ashangiliwe baada ya mechi.
Mashabiki walimzomea kocha Mdenmark Kim Poulsen baada ya mechi wakimuambia timu imemshinda na kumtaka aondoke.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Ivo Mapunda, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/Himid Mao dk56, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Frank Domayo, Hassan Dilunga/Salum Abubakar dk51, Mwinyi Kazimoto/Amri Kiemba dk51, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Mrisho Ngassa/Farid Mussa dk80.
Zimbabwe; Tapiwa Kapini, Ocean Mushere, Carrington Nyandemba, Obey Mureneheri/Misheck Mborai dk46, Themba Ndhlovu/Felix Chidungwe, Isaac Majari/Patson Jaure, Kapinda Wonder, Kundawashe Mahachi, Warren Dube/Nkosana Siwela, Lot Chiungwa/Gerald Ndhlovu na Simba Sithole.

Bao pekee la Future limefungwa na mshambuliaji wa Ruvu Shooting ya Pwani, Elias Maguri aliyeunganisha krosi ya chipukizi wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Juma Luizio.

TIMU ya soka ya pili ya taifa, Future Young Taifa Stars jioni hii imeifunga timu ya kwanza, Taifa Stars bao 1-0 katika mchezo maalum wa kirafiki Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Bao pekee la Future limefungwa na mshambuliaji wa Ruvu Shooting ya Pwani, Elias Maguri aliyeunganisha krosi ya chipukizi wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Juma Luizio.
Kabla ya kutia krosi, Luizio alimpokonya mpira beki mkongwe wa Yanga na mchezaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Kevin Yondan ambaye alianzishiwa na kipa wake, Ally Mustafa ‘Barthez’.

Elias Maguri kulia akipongezana na Juma Luizio baada ya kufunga leo Karume

Kwa ujumla Future waliihenyesha Stars inayoundwa na wachezaji nyota wa Tanzania wakiwemo Mrisho Ngassa, ambaye hii leo alishindwa kufurukuta.
Kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia ya Kenya alipewa nafasi kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Barthez lango la Stars na akadaka dakika 45 zote bila kuruhusu bao licha ua Future kushambulia kwa wingi.
Deo Munishi ‘Dida’ wa Yanga alianza katika lango la Future na kipindi cha pili akampisha Aishi Manula  wa Azam FC ambaye pia alifanya kazi nzuri.
Baada ya mechi, kocha wa Stars, Mdenmark Kim Poulsen alisema amevutiwa na uwezo wa kipa Mapunda na kwa ujumla mechi hiyo imemsaidia katika mkakati wake wa kuunda kikosi imara cha kudumu cha timu yake.
Rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi alikuwepo Uwanja wa Karume na baada ya mechi alizungumza na wachezaji akiwataka wafanye kazi nzuri ili wafurahie matunda ya uongozi wake.
Akawaambia Novemba 19 watacheza na Kenya, Harambee Stars, mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  
Future imeweka kambi hoteli ya Sapphire, wakati Stars ipo kambini Tansoma Hotel, zote maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam.

Timu za Taifa za Future Taifa Stars na Taifa Stars zinacheza kesho (Novemba 13 mwaka huu)

44714_ori_ivo_mapundaTimu za Taifa za Future Taifa Stars na Taifa Stars zinacheza kesho (Novemba 13 mwaka huu). Mechi hiyo ya kirafiki itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.
Mechi hiyo ni maalumu kwa Benchi la Ufundi la Taifa Stars linaloongozwa na Kim Poulsen kuangalia wachezaji kumi kutoka Future Taifa Stars watakaoongezwa katika Taifa Stars tayari kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayochezwa Novemba 19 mwaka huu jijini Arusha.
Watazamaji 300 tu wataruhusiwa kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini leo (Novemba 12 mwaka huu). Miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kuripoti ni kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia.

TANZANITE SASA NI KALI SANA

TANZANITETIMU ya taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) imefuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla ya mabao 15-1 baada ya leo (Novemba 9 mwaka huu) kuibugiza Msumbiji mabao 5-1.
Kwa mujibu wa kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura Mgoyo mabao ya Tanzanite katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini Maputo yalipatikana kupitia kwa Sherida Boniface alipiga matatu (hat trick) wakati mengine yalifungwa na Vumilia Maarifa na Donesia Minja.

Msafara wa Tanzanite ulioongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho Jumapili (Novemba 10 mwaka huu) saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.

Tanzanite inayofundishwa na Rogasian Kaijage itacheza mechi ya raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini. Mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Desemba 6 na 8 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika Afrika Kusini kati ya Desemba 20-22 mwaka huu.

USHINDI wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Oljoro na sare ya mabao 3-3 kati ya Azam FC na Mbeya City, kwa pamoja vimeifanya klabu ya soka ya Yanga kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya Bara hadi mwakani mzunguko wa pili utakapoanza.

MASIAUSHINDI wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Oljoro na sare ya mabao 3-3 kati ya Azam FC na Mbeya City, kwa pamoja vimeifanya klabu ya soka ya Yanga kujikita kileleni mwa Ligi Kuu ya Bara hadi mwakani mzunguko wa pili utakapoanza.
Yanga ilikuwa ikicheza na Oljoro kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeweza kusogea kutoka nafasi ya tatu iliyokuwa inashika awali hadi nafasi ya kwanza baada ya kufikisha pointi 28, huku sare ya mabao 3-3 ya Azam na Mbeya City ikizifanya timu hizo kufikisha pointi 27 kila moja. Timu zote zimecheza mechi 13.
Kwenye Uwanja wa Taifa, Yanga iliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 23 mfungaji akiwa Simon Msuva aliyeunganisha vyema krosi safi ya Haruna Niyonzima kutoka wingi ya kulia.
Baada ya kuingia kwa bao hilo, Oljoro walikuja juu lakini kitendo chao cha kucheza huku wakitumia nguvu nyingi kutaka kusawazisha kiliwasababishia wachezaji wao kadhaa kuumia kila mara huku Yanga wakiendelea kushambulia kwa kasi.
Mrisho Ngassa aliipatia Yanga bao la pili dakika ya 30 kwa shuti kali akiwa nje ya eneo la 18 la Oljoro ambalo kipa Damas Kugesha hakuweza kulizuia na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Yanga. Awali Kugesha alidhani Ngassa angetoa pasi mara baada ya kupokea pasi ya Frank Domayo kutoka katikati ya uwanja.
Mabao hayo ya Yanga yalidumu hadi mwamuzi Simon Mbelwa wa Pwani anapuliza filimbi ya kuashiria timu hizo ziende kupumzika. Kabla ya timu hizo kwenda mapumziko, Oljoro ilifanya mabadiliko kwa wachezaji Yusuph Mchogote na Babu Ally na nafasi zao kuchukuliwa na Deogratius Peter na Hamisi Saleh.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko baada ya kumtoa Hamisi Kiiza na nafasi yake ikachukuliwa na Jerry Tegete na mabadiliko hayo yaliongeza uhai kwa Yanga kwani dakika ya 53, Tegete aliipatia Yanga bao la tatu baada ya kupokea pasi nzuri ya Ngassa.
Ndani ya kipindi cha pili Oljoro ilifanya badiliko moja kwa kumtoa Sanu Mwaseba na nafasi yake kuchukuliwa na Amir Omar wakati Yanga waliwatoa Frank Domayo na Haruna Niyonzima na nafasi zao kuchukuliwa na Reliants Lusajo na Said Bahanuzi.
Mabadiliko hayo yaliongeza uhai kwa timu zote mbili lakini hadi dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliyoweza kupata bao baada ya mabadiliko hayo kufanywa licha ya Yanga kukosa mabao kadhaa ya wazi huku Oljoro nao wakifika langoni kwa Yanga mara chache.

Ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting

Azam-FC3Ushindi wa 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting Stars umeiwezesha Azam FC kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuuTanzania bara ikiwa imesalia na mchezo mmoja kumaliza mzunguko wa kwanza wa msimu huu wa 2013-2014.

 

Azam FC imepata ushindi huo na kufikisha pointi 26 sawa na Mbeya City ya mkoani Mbeya zikitofautiana kwa idadiya magoli huku timu zote zikiwa hazijapoteza hata mchezo mmoja, kwa matokeo ya jana timu ya Yanga inashukahadi nafasi ya tatu.

 

Mbeya City na Azam FC zitakutana katika mchezo wao wa mwisho wa kukamilisha hatua ya mzunguko wa kwanza,mchezo ambao kila timu itahitaji kushinda ili isiharibu rekodi yake pamoja na kuendelea kuongoza kwenye msimamowa ligi kuu, mechi hiyo itachezwa Nov 7 kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi na kurushwa moja kwa moja naAzam TV kupitia Chanel 10.

 

Katika mchezo wa huo uliozikutanisha Azam FC na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam Complex, Azam FC waliandika bao la kwanza mapema katika dakika ya kwanza ya mchezo kupitia kwa mshambuliaji Kipre Tchetche aliyeunganisha vizuri mpira wa  Joseph Kimwaga.

 

Azam FC ikiongoza 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, ilipata goli la pili mwishoni mwa kipindi cha kwanza katika dakika ya45, goli lililofungwa na mshambuliaji chipukizi Kimwaga kwa kichwa akimalizia mpira wa mwisho uliopigwa na Waziri Salum na kupeleka timu zote mapumziko Azam FC wakiongoza 2 huku Ruvu wakiwa hawajapata kitu.

 

Kipindi cha pili timu zote ziliingia kwa kasi Azam FC walifanya mabadiliko dakika ya 60 alitoka nahodha Himid Maonafasi yake ikachukuliwa na Jabir Aziz na dk 68 aliingia Farid Maliki kuchukua nafasi ya Kimwaga mabadiliko hayo yaliisaidia Azam FC kupata goli la tatu katika dakika ya 70 kupitia kwa Khamis Mcha aliyetumia vyema uzembe wabeki ya Ruvu na kumalizia mpira wa Kipre, goli hilo lilimaliza mchezo Azam FC wakiondoka na ushindi wa 3-0 dhidiya Ruvu Shooting.

 

Kipre amefikisha jumla ya magoli saba ya kufunga huku Kimwaga na Mcha wakifikisha magoli mawili kila mmoja.

 

Ruvu Shooting watajutia nafasi za wazi walizokosa katika nyakati tofauti wachezaji Hassan Dilunga, Cosmas Lewis, Elius Maguli na Said Dilunga walijaribu kupiga mashuti lakini yakaokolewa na kipa Mwadini Ally wa Azam FC na mengine kutoka nje hivyo kumaliza mchezo wakiwa hawajaziona nyavu za Azam FC.

 

Azam FC: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Morad, Aggrey Moris, Kipre Bolou, Joseph Kimwaga/Farid Maliki 68’, Himid Mao/Jabir Aziz 60’, Kipre Tchetche, Humphrey Mieno/Kelvin Friday 83’ na Khamis Mcha.

 

Ruvu Shooting: Abdul Juma, Michael Aidan, Stephano Mwasyika, Mangasini Mbonosi, Shaaban Sunza, Juma Seif Dion, Juma Nade, Hassan Dilunga, Said Dilunga, Elias Maguli na Cosmas Lewis/Raphael Kiara.

 

SOURCE: AZAM FC WEBSITE