simba 1 vs azam 2

Simba mpyaAzam-FC3BAO lililofungwa dakika ya 73 na mshambuliaji Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast limeiwezesha Azam FC kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Bara uliochezwa leo jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Tcheche alifunga bao hilo akiwa wingi ya kushoto ya uwanja huo na alipiga shuti kali la chinichini akiwa pembeni mwa uwanja (impossible angle) na mpira kutinga wavuni moja kwa moja. Kipa Abel Dhaira wa Simba pengine alidhani mfungaji alipiga mpira huo kama krosi kwenda kwa John Bocco, hivyo hakuwa makini kuzuia mpira huo wa kwanza.

Awali Tchetche alikuwa amepokea pasi kutoka kwa Salum Aboubakary ‘Sure Boy’ kutoka katikati ya uwanja. Sure Boy alipokea pasi baada ya mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki kupokonywa mpira jirani na katikati ya uwanja.

Ushindi huo wa Azam unaifanya timu hiyo kuishusha Simba kileleni mwa ligi hiyo na kuketi yenyewe ikiongoza kwa pointi 23 ilizopata baada ya kucheza mechi 11 kama ilivyo kwa Simba ambayo inapoteza mechi yake ya kwanza tangu kuanza kwa ligi hii msimu huu.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kushika nafasi ya pili ikiwa na pointi 20 ilizopata baada ya kucheza mechi 11, ambapo imeshinda mechi tano na kutoka sare tano. Simba imefunga mabao 21 na kufungwa mabao 10.

Bao la kwanza la Simba lilifungwa na Ramadhan Singano ‘Messi’ dakika ya 22 akimalizia pasi safi ya Zahor Pazi na kuamsha furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Baada ya kuingia kwa bao hilo, Simba ilionekana kutawala mchezo lakini Azam walizinduka kuanzia dakika ya 35 na kulishambulia lango la Simba kama nyuki na kufanikiwa kupata bao dakika ya 43 mfungaji akiwa ni Tchetche aliyemalizia kazi nzuri ya beki Erasto Nyoni.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko matokeo yalikuwa ni bao 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa Azam kufanya mabadiliko ambapo walimtoa beki Said Moradi na nafasi yake kuchukuliwa na David Mwantika ambaye aliweza kupunguza kasi ya mashambulizi ya Simba kwa kiasi fulani.

Dakika 10 baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, Simba ilifanya mabadiliko baada ya kuwatoa kwa mpigo Zahor Pazi na Amri Kiemba na nafasi zao kuchukuliwa na Sino Augustino na Edward Christopher.

Mabadiliko hayo hayakuweza kuisaidai Simba licha ya mara kadhaa kufika langoni kwa Azam lakini washambuliaji wake Sino Augustino na Mombeki hawakuwa makini kumalizia mipira mingi waliyokuwa wakipewa na viungo.

Tatizo la ukabaji wa nafasi ndilo lililoigharimu Simba na kumfanya Tchetche aifungie Azam bao la pili dakika ya 73.

Katika mchezo wake ujao, Simba itacheza na Kagera Sugar huku Azam ikipambana na Ruvu Shooting.

Advertisements

TANZANITES 10 VS MSUMBIJI 0

TIMU ya soka ya taifa ya wanawake kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, The Tanzanites imeifunga Msumbiji mabao 10-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia kwa mabinti wa umri huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.
Katika mchezo huo uliohudhuria na mashabiki wachache mno, hadi mapumziko, tayari Tanzanites walikuwa mbele kwa mabao 5-0. 

Neema Paul kushoto akishangilia na Theresa Yona baada ya kuifungia bao la kwanza Tanzania katika ushindi wa 10-0 jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya sita na Neema Paul aliyeunganisha pasi ya Theresa Yona, kutoka wingi ya kushoto, wakati mfungaji bora wa michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars iliyofanyika mwaka huu Nigeria, Shelder Boniface alifunga la pili dakika ya 24 baada ya kupangua ngome na kumpiga chenga hadi kipa.
Deonesia Daniel akafunga bao la tatu kwa shuti kali la mpira wa adhabu lililotinga moja kwa moja nyavuni dakika ya 32 na dakika ya 41, Amina Ali akafunga la nne kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la mita 18.

Wachezaji wa Tanzania wakishangilia mabao 10-0

Shelder Boniface akichezewa rafu na beki wa Msumbiji, Esperanca Malaita

Winga wa Tanzania, Theresa Yona akimtoka beki wa Msumbiji, Esperanca Malaita 

Theresa amepiga krosi

Shelder Boniface alifunga bao tamu sana, akipiga chenga mabeki watatu na kipa wao

Shelider Boniface alifunga bao ambalo lingekuwa la tano dakika ya 45, lakini refa Ines Niyonsara wa Burundi akakataa.
Kipindi cha pili The Tanzanites inayofundishwa na Rogasian Kaijage ilirudi na moto wake na kufanikiwa kupata bao tano, mfungaji Neema Paul aliyeunganisha krosi ya Theresa Yona.
Hatimaye Shelder alifunga bao la sita dakika ya 80 akimalizia mpira uliotemwa na kipa kufuatia shuti la Stumai Abdallah. 
Dakika ya 82 Tanzania ikapata bao saba kupitia kwa Amina Ali aliyefumua shuti kutoka katikati ya Uwanja. 

Kiungo wa Tanzania, Amina Ali akipambana na kiungo wa Msumbiji, Deolinda Gove 

  Theresa Yona alikuwa mwiba mkali leo kwa Msumbiji

          Amina Ali akiwaonyesha kazi wachezaji wa Msumbiji

                                    Kikosi cha Msumbiji leo

                                          Kikosi cha Tanzania leo

Mashabiki wakiisapoti timu ya Tanzania leo

Tanzanites walipata bao la nane dakika ya 86 kupitia kwa Deonesia Daniel aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, baada ya Shelder Boniface kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Dakika ya 89 Tanzania ilipata bao tisa kupitia kwa Amina Ali tena, ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo. Stumai Abdallah akaifungia Tanzania bao la 10 dakika ya 90.
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Celina Julius, Stumai Abdallah, Maimuna Said/Amina Hebron dk60, Fatuma Issa, Anastazia Anthony, Deonisia Daniel, Vumilia Maarifa, Amina Ali, Neema Paul, Shlder Boniface na Theresa Yona.
Msumbiji; Paulina Jambo/Catarina Francue dk50, Esperanca Malaita/Delice Assane dk52, Felismisa Moiane, Emma Paulino, Gilda Macamo, Deolinda Gove, Jessica Zunguene, Cidalia Cuta, Nelia Magate, LonicaTsanwane na Onesema David.

simba 3 yanga 3 live match

Simba mpya

DSC_0534

Dk 90+5 FULL TIME! Simba 3-3 Yanga 

 

Dk 83 GOOOOO…..! Gilbert Kaze anaipatia Simba bao la tatu akiunganisha krosi safi ya faulo iliyopigwa na Chollo. Simba 3-3 Yanga. 

 

Dk 72 Mpira umebadilika na Simba sasa wametawala mchezo. 

 

Dk 67 Mpira umesimama kwa muda baada ya Tambwe kuumia. 

 

Dk 64 Ngassa anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa. 

 

Dk 61 SUB: Yanga imefanya mabadiliko ametoka Kiiza ameingia Simon Msuva. 

 

Dk 60 YELLOW CARD…! Singano anaonyeshwa kadi ya njano. 

 

Dk 59 Simba wamebadilika na wanacheza soka safi sasa. 

 

Dk 57 GOOOOO…..! Joseph Owino anaipatia Simba bao la pili kwa kichwa akiunganisha mpira wa kichwa. Simba 2-3 Yanga. 

 

Dk 56 Simba inapata kona. 

 

Dk 54 GOOOOO….! Mombeki anaipatia Simba bao la kwanza akimalizia pasi nzuri ya Tambwe. Simba 1-3 Yanga. 

 

Dk 53 Niyonzima anakosa bao la wazi. 

 

Dk 48 SUB: Simba imefanya mabadiliko wametoka Abdulhalim Humud na Chanongo wameingia William Lucian na Said Hamisi. Simba 0-3 Yanga 

 

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA! 

 

Half time – Yanga 3 – 0 Simba 

 

Dk 45 GOOOOO….! Kiiza anaipatia Yanga bao la tatu akiunganisha vyema pasi ya Kavumbagu. Simba 0-3 Yanga. Simba 0-3 Yanga. 

 

Dk 43 Cannavaro anamchezea rafu Amisi Tambwe. 

 

Dk 41 Licha ya Yanga kuongoza kwa mabao 2-1, mashabiki watatu wa Yanga wamezimia na kupewa huduma ya kwanza. 

 

Dk 41 Chanongo anamchezea rafu Mbuyu Twite wa Yanga. 

 

Dk 38 Yanga wanapiga pasi 18 bila Simba kugusa. 

 

Dk 35 GOOOOOO…..! Kiiza anaipatia Yanga bao la pili akiunganisha mpira uliodokolewa na Kavumbagu aliyeugusa mpira uliorushwa na Mbuyu Twite. Simba 0-2 Yanga. 

 

Dk 32 YELLOW CARD…! Mkude wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano. 

 

Dk 26 David Luhende anakosa bao la wazi baada ya shuti lake kutoka nje kidogo ya lango la Simba. 

 

Dk 25 Kiiza anamchezea rafu Chanongo. 

 

Dk 24 Yanga inapata kona lakini Simba wanaokoa. 

 

Dk 23 Kavumbagu anakosa bao la wazi baada ya kipa Dhaira kuwahi kuudaka mpira. 

 

Dk 18 Kavumbagu anamchezea rafu Ramadhan Chanongo. 

 

Dk 15 YELLOW CARD…! Ngassa anaonyeshwa kadi ya njano kwa kuchelewesha muda. 

 

Dk 14 GOOOOOO….! Mrisho Ngassa anaipatia Yanga bao la kwanza akiunganisha vyema krosi ya Kavumbagu. Simba 0-1 Yanga 

 

Dk 13 Timu zinashambuliana kwa zamu lakini kazi ipo kwa Cannavaro na Mombeki. 

 

Dk 9 YELLOW CARD…! Mombeki anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Cannavaro. Rafu hii ni ile ya kwanza. 

 

Dk 7 Betram Mombeki wa Simba anapiga kichwa langoni kwa Yanga lakini kipa Ali Mustapha anaudaka mpira. 

 

Dk 7 Niyonzima anamchezea rafu Abdulhalim Humud wa Simba. 

 

Dk 4 Ngassa anapiga krosi safi langoni kwa Simba lakini Kiiza anachelewa kuunganisha. 

 

Dk 3 Jonas Mkude anamchezea rafu Mrisho Ngassa wa Yanga. 

 

Dk 2 Yanga wamecheza pasi 10 bila Simba kugusa. 

 

Dk 00 MPIRA UMEANZA! 

 

KIKOSI CHA YANGA KINACHOANZA

 

Barthez, Twite, Luhende, Cannavaro, Yondani, Chuji, Niyonzima, Domayo, Kavumbagu, Ngassa, Kiiza 

 

Subs: Deogratia Munisi, Juma Abdul, Oscar Joshua, Simon Msuva, Rajab Zahir, Jerson tegete, Nizar Khalifan 

 

KIKOSI CHA SIMBA KINACHOANZA

Dhaira, Cholo, Shamte, Kaze, Owino, Mkude, Singano, Humud, Mwombeki, Tambwe, Chanongo 

 

Subs: Abuu Hashim, Hassan Khatir, Issa Rashid, Zahoro Pazi, Amri Kiemba, Said Hamisi, William Lucian 

REFA aliyewahi kupigwa na wachezaji wa Yanga SC Machi mwaka jana timu hiyo ikifungwa 3-1

REFA aliyewahi kupigwa na wachezaji wa Yanga SC Machi mwaka jana timu hiyo ikifungwa 3-1 na Azam FC katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Israel Nkongo Mujuni ndiye atakayepuliza filimbi katika mchezo wa timu hiyo dhidi ya watani wa jadi, Jumapili. 
Nkongo alipigwa na wachezaji wa Yanga baada ya kumtoa kwa kadi nyekundu beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ akiwa tayari amempa kadi nyekundu kiungo Haruna Niyonzima pia. 
Stefano Mwasyika aliyehamia Ruvu Shooting alimtupia ngumi ya ‘kibondia’ Nkongo na Nadir Haroub ‘Canavaro’ alionekana kuhusika katika vurugu hizo wote wakafungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Mashabiki wa Yanga SC walifanya vurugu kubwa na kuvunja viti Uwanja wa Taifa siku hiyo.

Refa Israel Nkongo akikimbia wachezaji wa Yanga baada ya kutoa kadi nyekundu ya pili kwa Cannavaro

Aliyekuwa kipa wa Yanga, Shaaban Kado akidaka mbele ya John Bocco wa Azam

Mashabiki wa Yanga waling’oa viti ili kumshambulia Nkongo

Nahodha Nsajigwa akizuiwa na Polisi asimsogelee refa baada ya Niyonzima kupewa kadi nyekundu

Vijana mashabiki wa Yanga wakipelekwa rumande kwa tuhuma za kuvunja viti na chini Nkongo akitoka uwanjani kwa msaada wa Polisi

Canavaro akitolewa nje huku huku akilia na kocha wake Papic akimtuliza.

Papic akiwatuliza wachezaji na baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi

Canavaro akizuiwa na wenzake asimshushie kipondo refa huyo.

Polisi akiwa ameingia uwanjani ili kutuliza fujo hizo na kutoa ulinzi kwa refa huyo.

Mchezaji John Boko wa Azam FC akimtoka beki wa Yanga Haroub Nadir Canavaro.

Mashabiki wa Azam FC wakishangilia kwa furaha.

John Bocco akishangilia mara baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza.

Timu zikiingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo.

Yamepita hayo na Nkongo amepewa tena mechi ya Yanga. Marefa wote wanne walioteuliwa kuchezesha mechi hiyo ya watani wa jadi, Simba na Yanga mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wanatambuliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) 
Mbali na Nkongo atakayepuliza filimbi, wengine ni Hamisi Chang’walu atakayeshika kibendera upande wa jukwaa kuu na Ferdinand Chacha atakayeshika kibendera upande wa pili, wakati mezani atakaa Orden Mbaga.
Waamuzi hao wote wanne, kwanza wana uzoefu wa kutosha kustahili kuitwa wa kimataifa na wote wana beji za FIFA na hii pia si mara ya kwanza kwao kuongoza mechi za watani na kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakijitahidi kufanya vizuri.
Nkongo, Chang’walu na Mbaga wote ni wa Dar es Salaam, wakati Chacha anatokea Bukoba. 
Katika mchezo huo namba 63, kiingilio cha chini kitakuwa Sh. 5,000 ambako kuna viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648, wakati upande wa viti vya rangi ya bluu kiingilio ni Sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa itakuwa sh. 10,000, VIP C kiingilio ni sh. 15,000, VIP B itakuwa sh. 20,000 wakati VIP A yenye viti 748 tu tiketi moja itapatikana kwa sh. 30,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni katika vituo mbalimbali.
Vituo hivyo ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala, Uwanja wa Uhuru, na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.

TOUT Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo imetwaa taji la Super Cup la nchini humo baada ya kuifumua mabao 7-0 FC MK ya Kinshasa mjini Lubumbashi.

TOUT Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) leo imetwaa taji la Super Cup la nchini humo baada ya kuifumua mabao 7-0 FC MK ya Kinshasa mjini Lubumbashi.
Mabingwa hao mara nne Afrika tayario walikuwa mbele kwa mabao mawili hadi mapumziko, yaliyofungwa na mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu dakika ya 21 na kiungo wa Ghana, Daniel Nii Adjei dakika ya 33.

Mbwana Samatta akiwa ameinua taji la Super leo Lubumbashi

Dakika tano baada ya kuanza kipindi cha pili, Gladson Awako wa Ghana pia alifunga la tatu kabla ya ndugu yake Richard Kissi Boateng kufunga la nne dakika ya 66.
Adjei akafunga bao lake la pili katika mchezo huo dakika ya 68 kabla ya Herve Ndonga kufunga la sita dakika tatu baadaye na Mtanzania mwingine, Mbwana Samatta akafunga la saba dakika ya mwisho.
Ushindi huo mnono unakuja siku chache kabla ya kucheza Nusu Fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stade Malien ya Mali wiki ijayo, baada ya awali kushinda ugenini 2-1 katika mchezo wa kwanza.

 

 

 

 

YANGA YAICHAPA KAGERA SUGAR 2-1


Asante Ngassa

Chukua tano kwanza ….Asante!!
Kikosi cha Kagaera Sugar kilichoanza

Kikosi cha Yanga

Waamuzi wa mtanange huu

Waamuzi na Timu Kapteni wakiteta jambo muda mfupi kabla ya mpira kuanza

Benchi la Yanga kushoto ni Kocha mkuu

Benchi la Kagera Sugar

Dakika ya 2 Mpira ukirushwa kama kona na Kipa kuupangulia kwa adui na Hatimaye Mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngassa akafanikiwa kuipatia bao na hapa walikuwa wanashangilia bao hilo. Mpaka Mapunziko Yanga ilikuwa inaongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar. Habari na http://www.bukobasports.com

Wachezaji wa Yanga wakishangilia Baada ya kupata bao kupitia kwa Mrisho Ngassa

Kama Kawaida Yanga wanapofunga kufurahia kwa aina hii si ajabu

Raha ya Ushindi..jamani..

Asante Ngassa

Chukua tano kwanza ….Asante!!

Patashika Uwanjani..Baadhi ya Mashabiki waliojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Kaitaba.Kipindi cha pili dakika ya 49 Godfrey Wambura akaisawazishia bao timu yake na kufanya 1-1 na mtanange Kuchangamka sana kuliko kipindi cha kwanza..
Dakika ya 60 Hamis Kiiza akaiongezea bao Yanga na kufanya 2-1 Dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar.                                                                                           Hakuna kwenda popote!!

Kocha wa Kagera Sugar Mayanja
                                                        Kagera Sugar wakishangilia  baada ya kusawazisha bao dakika ya 49.

Mchezaji wa Kagera akitafuta wenzake kuwapa mpira kipindi cha pili
                                                                                Mashabiki wa Kagera Sugar
                                                                 Ni kama walitaka sare au Waifunge Yanga!!
                                                                           Mashabiki walijitokeza sana
                          KAZI NZURI: Wachezaji wa Yanga wakipongezana baada ya kupata bao la pili na la ushindi

wachezaji wa Yanga wakimpongeza Mwenzao Kiiza baada ya kuwapatia bao la ushindi

Safi…ndugu yangu Yanga sasa tunapanda…
                                                                                        Nyomi ilisheeni
                                                                      Kiiza akipongezwa na Mrisho Ngassa
                                                                                          Patashika kwenye goli la Yanga
                                                                            Majanga hapa kipindi cha pili..
                                                                            Kipa aliumia hapa wa Kagera

Kocha wa Kagera Bw. Mayanja akiojiwa na wahandishi wa Habari ambapo tuuma zote amezitupia kwa Mwamuzi aliyechezesha mtanange huo

Wadu na wapenzi wa Yanga wakifurahia ushindi huo
                                                                    Kiongozi wa Yanga nae akiojiwa kuhusu mtanange huo

Tumeshinda na huu ushindi ni muhimu kwetu …Tumepanda juu nafasi ya pili …ila mtanange ulikuwa mgumu sana

SIMBA SC jioni hii imezidi kupaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

SIMBA SC jioni hii imezidi kupaa kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao pekee la Simba SC katika mchezo huo limefungwa na kiungo Jonas Mkude dakika ya 62 na sasa Wekundu hao wa Msimbazi wanatimiza pointi 18 baada ya kucheza mechi nane.   

Simba mpya

 

  Simba SC inatarajiwa kuingia kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya      wapinzani wao wa jadi, Yanga SC Oktoba 20, Uwanja wa Taifa, Dar es  Salaam baada ya mechi ya leo.
 Uwanja wa Kaitaba, mabingwa watetezi Yanga SC wamepata ushindi wa  kwanza ugenini msimu huu baada ya kuilaza Kagera Sugar mabao 2-1,  hivyo kupaa hadi nafasi ya pili kwa kufikisha pointi 15.
 Yanga SC walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya pili mfungaji Mrisho  Ngassa aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kurushwa wa beki wa kulia  Mbuyu Twite.
 Baada ya bao hilo, Yanga walicharuka kusaka mabao zaidi, lakini Kagera  Sugar walisimama imara na kujizuia kuruhusu mabao zaidi.
 Hadi mapumziko, Yanga walikua mbele kwa bao hilo 1-0, lakini dakika ya  pili tu baada ya kuanza kipindi cha pili, mshambuliaji Godfrey Wambura  aliisawazishia Kagera baada ya kuuwahi mpira uliozuiliwa na mabeki wa  Yanga kufuatia krosi maridadi ya Paul Ngway.
 Yanga walicharuka baada ya bao hilo na kuzidisha mashambulizi langoni  mwa Kagera, hatimaye kufanikiwa kupata bao la ushindi dakika ya 59  mfungaji Hamisi Kiiza ambaye alimtoka beki Ernest Mwalupani baada ya  kupigiwa pasi ndefu na Mbuyu Twite.      
 Baada ya bao hilo, kasi ya mchezo iliongezeka kwa pande zote mbili,  Kagera wakisaka bao la kusawazisha na Yanga wakitaka mabao zaidi, lakini  hadi refa Hamad Kikumbo wa Dodoma anapuliza kipyenga cha kuhitimisha  mchezo huo, matokeo yalibaki 2-1.
 Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, David  Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’,  Mrisho Ngassa, Frank Domayo, Didier Kavumbangu, Hamisi Kiiza/Hussein Javu dk89 na Haruna Niyonzima/Simon Msuva dk60.   
Kagera Sugar; Agathon Anthony, Benjamin Asukile, Salum Kanoni, Maregesi Mwangwa, Ernest Mwalupani, George Kavilla/Rashid Roshwa dk78, Godfrey Wambura, Daudi Jumanne, Themi Felix, Suleiman Kibuta na Paul Ngway/Bukenya Kitagenda dk67.


DSC_0534

 

 

 

AZAM FC imepaa hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo JKT ya Tanga jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

AZAM FC imepaa hadi nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mgambo JKT ya Tanga jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Ushindi huo, unaifanya timu hiyo ya bilionea Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa itimize pointi 14, baada ya kucheza mechi nane, ikiwa sasa inazidiwa pointi moja tu na Simba SC iliyo kileleni, japokuwa Azam imecheza mechi moja zaidi. Yanga SC yenye pointi 12 inaangukia nafasi ya tatu

Nyuma kabisa ya Simba; Azam FC sasa ya pili Ligi Kuuazam252bvit1

Ushindi wa leo umetokana na mabao ya winga kinda aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili, Farid Malik dakika ya 66 na mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Kipre Herman Tchetche dakika ya 83.
Malik alifunga bao lake akiunganisha krosi maridadi ya beki wa kulia wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Erasto Nyoni, wakati raia wa Ivory Coast, Kipre Tchetche alifunga kwa penalti baada ya beki wa Mgambo, Ramadhan Kambwili kumuangusha Farid kwenye eneo la hatari.
Azam ingeweza kupata ushindi mnono zaidi kama si washambuliaji wake, Kipre na John Bocco kupoteza nafasi kadhaa nzuri za kufunga kwenye mchezo huo.  
Kikosi cha Azam FC leo kilikuwa; Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Brian Umony/Farid Malik, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Humphrey Mieno/Khamis Mcha, John Bocco na Farid Malik.
Mgambo JKT; Tony Kavishe, Daud Salum, Salum Mlima, Bakari Mtama, Bashiru Chanacha, Novat Lufunga, Nassor Gumbo, Mohamed Samatta, Mohamed Netto, Salum Gilla na Peter Malyanzi.
Katika mechi nyingine, mabao ya Juma Luizio dakika ya nne na saba yameipa Mtibwa Sugar ushindi wa 2-1 dhidi ya JKT Ruvu ambayo bao lake lilifungwa na Salum Machaku dakika ya 52, Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
JKT Oljoro imetoka sare ya 2-2 na Ruvu Shooting Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Mabao ya Oljoro yamefungwa na Nurdin Mohamed dakika ya 25 na Fikiri Mohamed dakika ya 64, wakati ya Ruvu yamefungwa na Elias Maguri dakika ya tatu na 40.
Mbeya City imeshinda ugenini, Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora mabao 3-1 dhidi ya wenyeji Rhino Rangers.