Simba watakuwa wakicheza wakitaka ushindi wa pili mfululizo katika ligi kuu ya Vodacom watakapokutana na Mtibwa Sugar leo hii katika uwanja wa taifa.

Simba-players-lift-shoulder-high-their-hero-Juma-KasejaSimba watakuwa wakicheza wakitaka ushindi wa pili mfululizo katika ligi kuu ya Vodacom watakapokutana na Mtibwa Sugar leo hii katika uwanja wa taifa. Simba pia watakuwa wakitafuta namna ya kulipa kisasi cha msimu uliopita ambao walifungwa mechi zote mbii na wakata miwa wa Turiani.
Huu ni mchezo wa kwanza wa Simba kucheza uwanja wa nyumbani msimu huu, wakiwa tayari wamecheza ugenini Tabora na Arusha katika michezo miwili ya kwanza ya msimu. Walishinda mechi yao ya kwana kwa kuwafunga JKT Oljoro 1-0 jijini Arusha shukrani kwa bao la Haroun Chanongo katika dakika ya 34 ya mchezo. 


Simba wamecheza mbili za kujipima nguvu kabla ya mchezo wa leo dhidi ya mabingwa wa Zanzibar KMKM na timu ya ligi ya daraja la kwanza, Lipuli. Wachezaji wake wote muhimu wapo vizuri kucheza akiwemo mchezaji mpya, nahodha wa zamani wa timu hiyo, Henry Joseph Shindika.

Mechi 3 zijazo za Simba: Mgambo JKT and Mbeya City (zote za nyumbani), JKT Ruvu (Ugenini)

Mtibwa pia itakuwa ikiutaka ushindi wa pili mfululizo katika VPL baada ya kupata ushindi wa kwanza kuwafunga wakata miwa wenzao, Kagera Sugar wiki mbili zilizopita. Chini ya makocha ambao wameishatumikia timu hiyo wakiwa wachezaji Mexime na Zuberi Katwila, watakuwa wakitafuta namna ya kuendeleza umwamba wao dhidi ya vijana wa mitaa ya msimbazi.


Mechi 3 zijazo za Mtibwa Sugar: Mbeya City (Nyumbani), Tanzania Prison na Ashanti United (Ugenini).

TAKWIMU ZA SIMBA VS MTIBWA: Simba imefungwa mechi mbili za mwisho ilizokutana na Mtibwa. Mtibwa Sugar hawajaruhusu wavu wao kuguswa katika mechi mbili zilizpita dhidi ya Simba.


Kikosi cha Simba katika mechi iliyopita ambacho kinaweza kuanza leo: Abel Dhaira, Nassor Chollo, Issa Rashid, Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Abdulhalim Humud, Amis Tambwe, Betram Mwombeki, Haroun Chanongo

Wachezaji muhimu: Amisi Tambwe na Betram Mwombeki (Simba). Simba watawategemea washambuliaji wao wawili wakati Mtibwa itategemea zaidi maujuzi ya Shaban Kisiga na Juma Luizio ambao pia wanaweza kuungana na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Hassan Mgosi.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s