Moja ya mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya kesho (Julai 27 mwaka huu) dhidi ya Uganda kuwania kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini ni kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.

Moja ya mikakati ya Taifa Stars kwenye mechi ya kesho (Julai 27 mwaka huu) dhidi ya Uganda kuwania kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Tatu za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini ni kushambulia kwa muda mwingi wa mchezo.tanzania_flag4STARS2

 
Kocha Kim Poulsen amesema maandalizi ya Taifa Stars jijini Mwanza kwa ajili ya mechi hiyo ambayo Uganda inaongoza kwa bao 1-0 yalikuwa mazuri, lakini mabao ni muhimu hivyo watashambulia bila kusahau kulinda lango lao.
 
“Unapocheza mechi za aina hii za nyumbani na ugenini, huku mwenyeji akiwa anaongoza mabao yana maana kubwa katika mechi. Mabao yanabadili mchezo na pia wachezaji kifikra,” amesema Kim akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Mt. Zion ambayo Stars imefikia.
 
Amesema katika mechi ya kwanza walitengeneza nafasi nyingi lakini hawakuzitumia, hivyo wamekuwa wakifanya mazoezi ya kushambulia, jinsi ya kutengeneza nafasi, na jinsi ya kumalizia.
 
“Hivyo tuko hapa (Kampala) kwa ajili ya kufunga, ni lazima tufunge ili tuweze kuendelea na mashindano. Lakini ngome yetu nayo ni lazima iwe makini ili kutoruhusu bao,” amesema Kim na kuongeza kuwa kikosi chake cha kwanza ni lazima kitakuwa mabadiliko kutoka na Mwinyi Kazimoto kuingia mitini na Shomari Kapombe kwenda kwenye majaribio Uholanzi.
 
Amesema angalau kutakuwa na mabadiliko kwa kuingiza sura mbili mpya katika kikosi cha kwanza, na kuongeza kuwa wachezaji wanafahamu umuhimu wa mechi hiyo kwani timu ikienda kwenye Fainali za CHAN itakuwa manufaa kwao binafsi.
 
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefanya mazoezi ya mwisho leo jioni Uwanja wa Mandela ulioko Namboole ambao utatumika kwa ajili ya mechi hiyo kesho.
 
Mechi hiyo itaanza saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki na itachezeshwa na waamuzi kutoka Madagascar wakiongozwa na Kanoso Abdoul Ohabee wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Andirvoavonjy Pierre Jean Eric. Mwamuzi msaidizi namba mbili ni Jinoro Velomanana Ferdinand huku Andriamiharisoa Hubert Marie Bruno akiwa mwamuzi wa mezani (fourth official). Kamishna wa mechi hiyo namba 38 ni Ismail Kamal kutoka Ethiopia.
 
Stars inatarajiwa kupangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Salum Abubakar, Frank Domayo, John Bocco, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.

Exclusive: Joseph Owino is back

                                                                                                     bao206af-blogger-image-1710630466d36cf-blogger-image-1056270426

Beki wa URA ya Uganda Joseph Owino anategemea kujiunga na timu ya Simba ambayo alikuwa akiichezea misimu mitatu iliyopita kabla ya kujiunga na Azam kutoka Mbagala Jijini Dar-es-salaam.


Beki huyo alirejea kwao Uganda baada ya kupata majeraha na kushindwa kucheza katika timu za Simba na Azam akiwa kwenye kiwango chake kama alivyokuwa akicheza kabla ya kuumia.
 
Baada ya kurudi Uganda Owino alitibiwa na kupona vizuri kisha kujiunga na URA ambayo amekuwa mpaka sasa. Viongozi wa benchi la ufundi la Simba Kocha Abdallah King Kibaden, msaidizi wake Julio ana meneja Moses Basena wote waliridhishwa na kiwango cha Owino na hivyo kupeleka maombi kwa uongozi kumsajili mchezaji huyo. 
 
Viongozi wa Simba sasa wapo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha dili hilo na kumrudisha Owino msimbazi, sehemu ambayo aliichezea kwa mafanikio makubwa sana alipojiunga na timu miaka kadhaa iliyopita.

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mdenmark Kim Poulsen amesema kwamba ameiandaa vyema timu yake kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Uganda, The Cranes kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazohusisha wachezaji wanaocheza Ligi za nchini mwao pekee.

Mei 26, 2012 STARS

Taifa6

Tanzania 0 – 0 Malawi (Kirafiki)

Juni 2, 2012

Ivory Coast 2 – 0 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)

Juni 10, 2012

Tanzania 2 – 1 Gambia (Kufuzu Kombe la Dunia)

Juni 17, 2012

Msumbiji 1 – 1 Tanzania  (Tanzania ilitolewa kwa penalti kufuzu Mataifa ya Afrika)

Agosti 15, 2012

Botswana 3 – 3 Tanzania (Kirafiki)

Novemba 14, 2012

Tanzania 1-0 Kenya (Kirafiki)

Desemba 22, 2012

Tanzania 1-0 Zambia (Kirafiki)

Januari 11, 2013

Tanzania 1-2 Ethiopia (Kirafiki)

Februari 6, 2013

Tanzania 1-0 Cameroon (Kirafiki)

Machi 24, 2013

Tanzania 3-1 Morocco (Kufuzu Kombe la Dunia)

Juni 2, 2013

Sudan 0 – 0 Tanzania (Mechi ya kirafiki Ethiopia)

Juni 8, 2013 

Morocco 2-1 Tanzania (Kufuzu Kombe la Dunia)

Juni 16, 2013

Tanzania 2-4 Ivory Coast (Kufuzu Kombe la Dunia)

 

Kim ameyasema hayo leo asubuhi katika Mkutano wa pamoja na mpinzani wake, Mserbia Milutin Sredojvic ‘Micho’ wa The Cranes na Waandishi wa Habari kuhusu mchezo huo wa kesho uliofanyika katika hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam.

Tanzania na Uganda zipo katika kambi jirani, Kariakoo, Dar es Salaam, Stars wakiwa hoteli ya Tansoma na Cranes hoteli ya Sapphire Court, maeneo ya Gerezani. 

Makocha wote waliezea ubora wa wapinzani, lakini wakasisitiza kuwa wanaingia uwanjani kuhakikisha wanashinda ili kujiweka katika mazingira mazuri kwa ajili ya mechi ya marudiano itakayochezwa Kampala wiki mbili zijazo.

Kim alisema Uganda ndiyo inayoongoza kwa ubora wa viwango vya FIFA katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati, hivyo ni changamoto kwao ingawa wachezaji wake tayari wamejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.

Naye Micho aliyefuatana na nahodha wake, Hassan Wasswa alisema Taifa Stars imekuwa ikifanya vizuri tangu iwe chini ya Kim, na itakuwa na wachezaji tisa wa kikosi cha kwanza kinachocheza mechi za mchujo za Kombe la Dunia wakati kwa upande wake atakuwa na wachezaji wawili tu.

Mchezo wa kesho utakuwa wa 13 kwa Kim tangu aanze kuinoa Stars, akirithi mikoba ya Mdenmark mwenzake, Jan Borge Poulsen baada ya kupandishwa kutoka timu za vijana. 

Katika michezo hiyo 13, Kim ameiwezesha Stars kushinda mechi tano, sare nne na kufungwa nne, ikifunga jumla ya mabao 16 na kufungwa 16 katika mechi zote hizo, kipigo kikubwa zaidi kikiwa 4-2 nyumbani mwezi uliopita kutoka Ivory Coast na ushindi mnono ukiwa wa 3-1 kutoka Morocco Machi mwaka huu.

SIMBA SC tayari ipo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

SIMBA SC tayari ipo wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ambako itacheza mchezo mmoja wa kujipima nguvu na Kahama United Jumapili kwenye wa Manispaa wilayani humo.
Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Joseph Itang’are ‘Kinesi’ amesema kwamba baada ya mchezo huo wa Jumapili, timu itaelekea Musoma mkoani Mara kucheza mechi moja zaidi.

Amesema mjini Musoma watacheza na kombaini ya Musoma kwenye Uwanja wa Karume Jumatano, yaani Julai 17 na baada ya hapo timu itarejea Dar es Salaam.
URA ya Uganda inatarajiwa kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kucheza na Simba SC Julai 20, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam 
Simba, kabla ya kwenda Kahama ilikwenda Katavi ambako ilicheza mechi mbili na kushinda zote, 3-1 dhidi ya Rhino FC ya Tabora na 2-1 dhidi ya kombaini ya Katavi kwenye Uwanja wa wazi wa Katavi mkoani humo. 
Simba SC, ambayo ilikuwa Katavi kwa mwaliko wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika mchezo wake wa kwanza, mabao yake yalifungwa na Edward Christopher mawili na moja Nahodha mpya, Nassor Masoud ‘Chollo’ na mchezo uliofuata mabao yalifungwa na Kun James mshambuliaji aliye katika majaribio kutoka Al Ahly Shandi ya Sudan Kusini na beki Mganda, Samuel Ssenkoom aliyesajiliwa kutoka URA.

YANGA SC imekamilisha ziara yake ya Kanda ya Ziwa kwa sare.

YANGA SC imekamilisha ziara yake ya Kanda ya Ziwa kwa sare ya bila kufungana na wenyeji Rhino FC iliyopanda Ligi Kuu msimu huu kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora jioni hii.
Pamoja na sare hiyo, Yanga SC ilishindwa kucheza vyema kwenye Uwanja huo dhidi ya wenyeji, Rhino timu inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kutokana na ubovu wa Uwanja.

Mabingwa hao wa Bara, pamoja na hali hiyo mbovu ya Uwanja walijitahidi kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga mabao, lakini washambuliaji wake waliendeleza kile kinachojulikana mbele ya wapenzi wao, kushindwa kutumbukzia mipira nyavuni.
Wote Didier Kavumbangu, Jerry Tegete, Shaaban Kondo na Said Bahanuzi walikosa mabao ambayo huwezi kuamini, na kutokana na ukweli kwamba hao ndio washambuliaji pekee wa timu hiyo, maana yake wanahitaji kuboresha safu hiyo. 
Awali, katika ziara hiyo ya kujiandaa na msimu mpya, Yanga inayofundishwa na kocha Mholanzi, Ernie Brandts ilitoka sare ya 1-1 mjini Mwanza Julai 6 na Express ya Uganda kabla ya kufungwa 2-1 mjini Shinyanga na timu hiyo siku iliyofuata.
Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, bao la Yanga lilifungwa na kiungo Hamisi Thabit aliyesajiliwa kutoka African Lyon dakika ya 40, wakati Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, bao la kufutia machozi lilifungwa na Shaaban Kondo, baada ya mpira wa kurushwa wa Mbuyu Twite.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Yanga kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Rajab Zahir/Ibrahim Job, Mbuyu Twite, Salum Telela, Nizar Khalfan, Hamisi Thabit/Abdallah Mnguli, Didier Kavumbangu, Jerry Tegete/Shaaban Kondo na Said Bahanuzi.

Tanzania-taifa stars

DSC_0178

Waamuzi hao ni Thierry Nkurunziza atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake watakuwa Jean Claude Birumushahu naPascal Ndimunzigo. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni pacifique Ndabihawenimana.
Kamishna wa mechi hiyo Gebreyesus Tesfaye kutoka Eritrea. Tesfaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Eritrea na mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya CHAN.
CAF pia imeteua Leslie Liunda wa Tanzania kuwa Kamisaa wa mechi kati ya Burundi na Sudan itakayochezwa jijini Bujumbura.
Mechi hiyo ya kwanza ya mchujo ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) itafanyika keshokutwa (Julai 7 mwaka huu). Liunda anatarajia kuondoka leo usiku (Julai 5 mwaka huu) kwenda Bujumbura.
Wakati huo huo: Jjumla ya makocha wa mpira wa miguu na walimu 28 kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na shule za msingi na sekondari wameteuliwa kuhudhuria kozi ya FIFA 11 For Health inayoanza keshokutwa (Julai 7 mwaka huu) Homboro mkoani Dodoma.
Kozi hiyo itakayomalizika Julai 20 mwaka huu itakuwa chini ya ukufunzi wa Rogasian Kaijage ambaye pia ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake (Twiga Stars).
Washiriki ni Abdul Mikoroti (Shule ya Msingi Nzasa), Baltazar Kagimbo (Shule ya Msingi Tabata Jica), Baraka Baltazar (Shule ya Msingi Muhimbili), David Kivinge (Shule ya Msingi Temeke), Dismas Haonga (Tambaza Sekondari), Exuperus Kisaka (Shule ya Msingi Mavurunza) na Hadija Kambi (Shule ya Msingi Karume).
Hamis Chimgege (Shule ya Msingi Tusiime), Hobokela Kajigili (Shule ya Msingi Buguruni), Issack Mhanza (Shule ya Msingi Airwing), Job Ndugusa (Shule ya Msingi Upanga), John Sebabili (TFF), Lutta Rucharaba (Shule ya Msingi Montfort), Maua Rahidi (Shule ya Msingi Uhuru Wasichana), Michael Bundala (TFF) na Mussa Kapama (Shule ya Msingi Bunju ‘A’).
Priscus Silayo (Shule ya Msingi J.K. Nyerere), Peter Manyika (TFF), Rajabu Asserd (Shule ya Msingi Mtoni Kijichi), Raphael Matola (TFF), Raymond Rupia (St. Anne Maria Academy), Renatus Magolanga (Ulongoni Sekondari), Ruth Mahenge (Shule ya Msingi Chang’ombe), Said Pambaleo (TFF), Sebastian Nkoma (TFF), Titus Michael (TFF), Wane Mkisi (Jangwani Sekondari).