20130326-205906.jpg

Na fzakar

WACHEZAJI wawili wa Simba SC, kipa Abbel Dhaira na kiungo Mussa Mudde hawatashiriki mechi ya kesho ya klabu yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar kutokana na kukwama nchini Ghana.
Wawili hao, walikuwa Liberia mwishoni mwa wiki na timu ya taifa ya Uganda, The Cranes iliyokwenda kumenyana na wenyeji wao hao katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil.
Hata hivyo, wakiwa njiani kurejea nchini kujiunga na klabu yao, imeelezwa kwamba wamekwama Ghana.
“Wamekwama Ghana,”alisema Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga alipozungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii, ingawa hakuwa tayari kueleza kwa undani juu ya kilichowakwamisha wachezaji hao.
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, inatarajiwa kuendelea kesho kwa mechi mbili, mabingwa watetezi Simba wakiwa wageni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 3,000 unatarajiwa kushuhudia mechi yenye ushindani mkali kutokana na uwezo wa wachezaji wa pande zote mbili.
Mechi nyingine itapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam kati ya wenyeji Azam na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
Tayari wachezaji wa Simba SC waliokuwa na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyomenyana na Morocco mjini Dar es Salaam Jumapili na kushinda 3-1 wapo Bukoba kwa ajili ya mchezo huo.
Hao ni kipa na Nahodha, Juma Kaseja, mabeki Nassor Masoud ‘Chollo’, Shomary Kapombe na viungo Mrisho Ngassa na Amri Kiemba.
Kiungo mwingine wa Simba SC aliyekuwa na Taifa Stars Jumapili, Mwinyi Kazimoto yeye hajaenda Bukoba kwa sababu hayumo kwenye mipango ya kocha Mfaransa, Patrick Liewig kwa sasa.
Simba SC inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu kwa sasa kwa pointi zake 34, ikiwa nyuma ya Azam yenye pointi 37, wakati Yanga SC yenye pointi 48 inaongoza ligi hiyo.

Advertisements

20130324-103345.jpg

Dk 90+4 FULL TIME! TAIFA STARS 3-1 MOROCCO

Dk 90+3 Morocco inapata bao. TAIFA STARS 3-1 MOROCCO

Dk 90 Taifa Stars imefanya mabadiliko, ametoka Samatta ameingia John Bocco.

Dk 87 Ulimwengu anaumia baada ya kuangushwa na beki wa Morocco. Anatibiwa na kurudi uwanjani.

Dak 86: Taifa Stars 3-0 Morocco

Dk 80 RED CARD..! Achchakir Abderrahm wa Morocco anaonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumtolea lugha chafu mwamuzi Helder Martins wa Angola.

Mbwana Samatta anaiandikia Tanzania bao la 3.

Dk 68 Morocco inafanya mabadiliko, ametoka Barrada Abdelaziz ameingia El Bahri Brahim.

Dk 67 GOOO….! Samatta anaifungia Taifa Stars bao la pili akimalizia mpira aliopenyezewa kutoka katikati ya uwanja baada mbio mabeki wa Morocco.

Dk 65 Yondani anavuruga vizuri mpira wa Eladoua Issam wa Morocco aliyekuwa anaenda kufunga.

Dak 63: Athuman Iddi anaingia kuchukua nafasi ya Mrisho Ngassa

Dk 61 Ngassa anachelewa kuunga krosi safi ya Samatta.

Dk 50 Taifa Stars inalishambulia zaidi lango la Morocco, uwepo wa Ulimwengu umeongeza kasi ya ushambuliaji ya Taifa Stars.

Dk 45 GOOO….! Thomas Ulimwengu anaifungia Taifa Stars bao la kwanza baada ya kuuwahi mpira ulioshindwa kuokolewa na mabeki wa Morocco na kufunga. TAIFA STARS 1-0 MOROCCO

Dk 45 Taifa Stars inafanya mabadiliko, ametoka Mwinyi Kazimoto ameingia Thomas Ulimwengu.

Dk 45 KIPINDI CHA PILI KIMEANZA!

Dk 45 HALF TIME! TAIFA STARS 0-0 MOROCCO.

Dk 45 Barrada Abdelaziz anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Samatta.

Dk 41 Beki wa Taifa Stars, Kelvin Yondan amejitahidi kuharibu mipira mingi ya adui.

Dk 41 Beki wa Taifa Stars, Kelvin Yondan amejitahidi kuharibu mipira mingi ya adui.

Dk 38 Eladoua Issam wa Morocco anapiga kichwa chepesi kinachotoka nje kidogo ya lango la Taifa Stars.

Dak 35: Starz 0 – 0 Morocco

Dk 33 Beki wa Taifa Stars, Shomari Kapombe anaichambua ngome ya Morocco na kupiga shuti kali linalotoka nje ya lango.

Dk 31 Kaseja anadaka shuti kali la Achchakir Abderrahm.

Dk 25 Straika wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anakosa bao la kichwa akiunga krosi ya Mrisho Ngassa.

Dk 24 Kipa wa Taifa Stars, Juma Kaseja anaokoa shuti kali lililoelekezwa langoni kwake.

Dk 18 Kiungo wa Taifa Stars, Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ anapiga shuti kali kuelekea lango la Morocco lakini kipa Lamyaghri Nadir anaudaka mpira.

Dk 14 Beki wa Taifa Stars, Aggrey Morris anaukosa mpira kwa kichwa kuelekea lango la Morocco baada ya Taifa Stars kupata kona.

Dakika ya 9 timu zinashambuliana sana huku zikisomana.

Mpira umeanza hapanuwanja wa taifa.

Kikosi cha Taifa Stars kitakachoanza dhidi ya Morocco:1.Juma Kaseja2.Erasto Nyoni3.Shomari Kapombe4. Aggrey Morris5. Kelvin Yondani6. Frank Domayo7. Mrisho Ngasa8. Sureboy9. Mbwana Samatta10. Amri Kiemba11. Mwinyi Kazimoto

20130323-222803.jpg

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC leo wamelazimishwa sare ya kufungana na 1-1 na Rhino Rangers ya Tabora iliyopanda Ligi Kuu katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora, maalum kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba Jumatano,
Simba SC ambayo katika mchezo wake uliopita wa kirafiki iliifunga Singida United mabao 4-0, katika mchezo wa leo, bao lake limefungwa na Edward Christopher Shijja, mfungaji bora wa Kombe la BancABC Sup8R.
Katika mchezo uliopita uliofanyika kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida, mabao ya mabingwa hao wa Bara, yalitiwa kimiani na Rama Kipalamoto, Mselemu Salum, Omar Waziri ‘Inzaghi’ na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Simba SC ambayo imewapumzisha wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza na kuamua kutumia chipukizi waliopandishwa kutoka kikosi cha pili, leo pia ilicheza soka ya kuvutia na kupoteza nafasi kadhaa za kufunga mabao zaidi.
Kocha Mfaransa, Patrick Liewig alitoa pendekezo la kutolewa kwa wachezaji ‘mafaza’ katika kikosi chake, kwa kuwa hawamsikilizi.
Miongoni mwa waliotengwa ni wachezaji hodari na vipenzi vya mashabiki kama Amir Maftah, Juma Nyosso, Haruna Moshi ‘Boban’ na Mwinyi Kazimoto.
Wachezaji hao makinda walicheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu wiki mbili zilizopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sasa timu hiyo inaelekeza nguvu zake katika mechi mbili za kanda ya Ziwa, ikianza na Kagera na baadaye Toto African mjini Mwanza wiki ijayo, huku wapenzi wengi wakiwa na imani na yosso wao hao.
Simba itaondoka kesho asubuhi kuelekea Bukoba tayari kwa mechi na Kagera Jumatano.
Kwa sasa, Simba SC inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu, ikiwa na pointi 34, tatu nyuma ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili wakati Yanga SC wapo jirani kabisa na ubingwa kwa pointi zao 48 ligi ikiwa imebakiza mizunguko sita kutia nanga.
Simba SC inapambana hata kama itapoteza ubingwa, basi iipiku Azam FC katika nafasi ya pili.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba kilikuwa; Abuu Hashim, Emily, Hassan Hassan, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Ndemla, Abdallah Sesemea, Rashid Ismail, Christopher Edward, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Haroun Chanongo.

Simba sport club

KATIKA kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba Jumatano, Wekundu wa Msimbazi, Simba SC leo wamecheza mchezo wa kirafiki mjini SIngida na kutoa adhabu kali ya kipigo cha mabao 4-0 kwa wenyeji, Singida United.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida, mabao ya mabingwa hao wa Bara, yalitiwa kimiani na Rama Kipalamoto, Mselemu Salum, Omar Waziri ‘Inzaghi’ na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Simba SC ambayo imewapumzisha wachezaji wake wengi wa kikosi cha kwanza na kuamua kutumia chipukizi waliopandishwa kutoka kikosi cha pili, leo ilicheza soka ya kuvutia mno.
Mashabiki wa soka mjini Singida walikuwa wakishangilia kwa nguvu burudani ya soka ya ‘Kibareclona’ na kupiga kelele timu hiyo iachane na magwiji wasio na nidhamu na kuwekeza zaidi kwa yosso hao.
Kocha Mfaransa, Patrick Liewig alitoa pendekezo la kutolewa kwa wachezaji ‘mafaza’ katika kikosi chake, kwa kuwa hawamsikilizi.
Miongoni mwa waliotengwa ni wachezaji hodari na vipenzi vya mashabiki kama Amir Maftah, Juma Nyosso, Haruna Moshi ‘Boban’ na Mwinyi Kazimoto.
Wachezaji hao makinda walicheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu wiki mbili zilizopita dhidi ya Coastal Union ya Tanga na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sasa timu hiyo inaelekeza nguvu zake katika mechi mbili za kanda ya Ziwa, ikianza na Kagera na baadaye Toto African mjini Mwanza wiki ijayo, huku wapenzi wengi wakiwa na imani na yosso wao hao.
Kwa sasa, Simba SC inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu, ikiwa na pointi 34, tatu nyuma ya Azam FC inayoshika nafasi ya pili wakati Yanga SC wapo jirani kabisa na ubingwa kwa pointi zao 48 ligi ikiwa imebakiza mizunguko sita kutia nanga.
Simba SC inapambana hata kama itapoteza ubingwa, basi iipiku Azam FC katika nafasi ya pili.
Katika mchezo wa leo, kikosi cha Simba kilikuwa; Abuu Hashim, Haruna Shamte, Waziri Omar, Hassan Hassan, Hassan Khatib, Jonas Mkude, William Lucian ‘Gallas’/Said Mangela, Mselem Salum, Christopher Edward, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Marcel Kahezya/Haroun Chanongo.

20130320-221931.jpg

AZAM FC imeanza vyema Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF)

AZAM FC imeanza vyema Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF), baada ya usiku huu kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Barrack Young Controllers katika mchezo wa kwanza wa hatua hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Antonette Tubman Monrovia, Liberia.
Kwa matokeo hayo, Azam sasa itahitaji hata sare tu ili kusonga mbele, Raundi ya Tatu na ya mwisho ya mchujo kabla ya hatua ya makundi.
Shujaa wa Azam FC leo alikuwa ni Seif Abdallah Karihe aliyefunga bao la ushindi dakika ya 90, kufuatia kazi nzuri ya Khamis Mcha ‘Vialli’.
Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Farouk Mohamed kutoka Misri, hadi mapumzikko, B.Y.C. walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na
Azam wangeweza kuondoka uwanjani baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza wakiwa wana mabao, kama wangeweza kutumia nafasi nzuri takriban sita walizopata.

20130317-174359.jpg

Young African

Dk 90 FULL TIME! YANGA 1-0 RUVU

Dk 83 Ruvu imefanya mabadiliko, ametoka Ayoub Kitala ameingia Raphael Kyala.

Dk 80 Yanga imefanya mabadiliko, ametoka Nizar ameingia Didier Kavumbagu.

Dk 78 Mangasini wa Ruvu anamchezea vibaya Nizar wakati akiwa katika harakati za kufunga. Nizar hawezi kuendelea na mchezo.

Dakika ya 75, Ruvu Shooting 0 – 1 Young AfricansDk 72 Yanga inatawala mchezo kwa kucheza mpira wa pasi nyingi.

Dakika ya 60, Ruvu Shooting 0 – 1 Young Africans

Dk 56 Ruvu wanafanya mabadiliko, ametoka Gideon Tepo ameingia Paul Ndauka.

Dk 55 Kiiza anashindwa kuunga kwa kichwa krosi ya Nizar.

Dk 50 Mangasini Mangasini wa Ruvu anampiga kiwiko Domayo lakini mwamuzi hajaona.

Wakati wa mapumziko Yanga ilifanya mabadiliko, ametoka Joshua ameingia David Luhende.

Dakika ya 48, Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la kwanza
Ruvu Shooting 0 – 1 Young Africa

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, Ruvu Shooting 0 – 0 Young Africans

Dk 45 HALF TIME! YANGA 0-0 RUVU.

Dk 43 Nizar wa Yanga anayecheza kama straika leo, anaonekana amechoka na kushindwa kuziwahi pasi na krosi nyingi zinazopigwa eneo lake.

Dk 39 Kipa wa Ruvu, Benjamin Haule anadaka kwa ustadi krosi ya Msuva huku Nizar akiwa tayari kuiunganisha.

Dk 36 Beki wa Yanga, Oscar Joshua anaonyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Jacob Adongo baada ya kumchezea rafu Said Dilunga.

Dakika ya 30, Ruvu Shooting 0 – 0 Young Africans

Dk 28 Said Dilunga wa Ruvu anakosa bao la wazi akiwa amebaki na kipa wa Yanga.

Dk 25 Ruvu wanapata kona baada ya Cannavaro kuutoa mpira nje. Kona isiyo na madhara imepigwa.
Dk 23 Mbuyu Twite wa Yanga anachezewa faulo na Said Dilunga.

Dk 22 Cannavaro anamchezea rafu Said Dilunga wa Ruvu.

Dk 19 Yanga imeongeza mashambulizi langoni kwa Ruvu. YANGA 0-0 RUVU.

DK 15, Ruvu Shooting 0-0 Yanga

Dk 10 Beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amemchezea faulo Abrahman Musa wa Ruvu. Timu zinashambuliana kwa zamu.

Dk 8 Kipa wa Yanga, Ally Mustapha ‘Barthez’ anapangua shuti kali la Michael Aidan wa Ruvu lililopigwa kutoka nje ya eneo la hatari.

Dk 7 Frank Domayo wa Yanga anachezewa faulo na Ayoub Kitala wa Ruvu.

Dk 4 Hamis Kiiza wa Yanga anapiga shuti kali langoni kwa Ruvu akiunganisha pasi ya Nizar Khalfani lakini kipa Benjamin Haule anaudaka mpira.

Mpira ndio umeanza hapa Uwanja wa Taifa kati ya Ruvu Shooting Vs Young Africans

Wachezaji wa timu zote na watazamaji wamesimama kwa dakika moja kuomboleza kifo cha kocha na mchezaji wa zamani wa Pan African marehemu mzee Athuman Chilambo.

Young Africans line-up to face Ruvu Shooting today:
1.Ally Mustafa ‘Barthez’
2.Juma Abdul
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub ‘Cannavaro’
5.Mbuyu Twite
6.Athumani Idd ‘Chuji’
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Nizar Khalfani
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Subs:
1.Said Mohamed
2.Shadrack Nsajigwa
3.David Luhende
4.Nurdin Bakari
5.Said Bahanuzi
6.Jerson Tegete
7.Didier Kavumbagu

RUVU SHOOTING: Benjamin Haule, Michael Aidan, Mau Bofu, Ibrahim Shaban, Mangasini Mangasini, Gideon Tepo, Ayoub Kitala, Ernest Ernest, Hassan Dilunga, Said Dilunga, Abrahman Musa

20130316-111733.jpg

20130316-111742.jpg

20130316-111957.jpg

KOCHA wa Simba, Patrick Liewig ametoa onyo kali kwa nyot

KOCHA wa Simba, Patrick Liewig ametoa onyo kali kwa nyota wake kwa kusema hakuna mchezaji anayeweza kuwa juu ya timu hiyo.
Kauli hiyo imekuja, baada ya hali ya nidhamu kwa wachezaji wa Simba kuwa mbovu na kuchangia timu hiyo kupata matokeo mabaya kwenye ligi.
Mfaransa huyo alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa tatizo hilo ameona zaidi kwa wachezaji ‘mafaza’
Hali ambayo imemlazimu kutumia wachezaji watano hadi sita vijana kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
“Nafikiri kama nidhamu itakuwa mbovu kwenye timu. Kamwe hatuwezi kufikia malengo ambayo tumejiwekea.”
“Kwa hiyo ni sahihi kwangu kwenda na wachezaji ambao wananielewa ambacho wanatuma kukifanya uwanjani.”
“Hakuna mchezaji anayeweza kuwa juu ya timu.” alisema kocha huyo aliyerithi mikoba ya Mserbia Milovan Cirkovic.

20130315-112350.jpg