13

 

KAMA ingekuwa ni ndondi, leo Tanzania wangetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Afrika, baada ya kuwapiga Zambia, lakini katika soka, haiku hivyo.

Tanzania, Taifa Stars leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika michezo ya kirafiki baada ya kuifunga Zambia 1-0, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo wa leo, hadi mapumziko, tayari Stars ambayo Novemba 14, mwaka huu iliifunga 1-0 Kenya, Uwanja wa CCM Kirumba, walikuwa mbele kwa bao 1-0 lililowekwa kimiani na kiungo mshambuliaji Mrisho Khalfan Ngassa.

Ngassa, anayecheza kwa mkopo Simba SC akitokea Azam FC, zote za Dar es Salaam, alifunga bao hilo dakika ya 45, akimalizia pasi nzuri ya kiungo wa Simba SC, Mwinyi Kazimoto.

Stars ilicheza vizuri na kwa umakini wa hali ya juu kipindi cha kwanza, na kufanikiwa kuwabana mabingwa hao wa Afrika wanaojiandaa kwenda kutetea taji lao nchini Afrika Kusini mapema mwakani.

Kipindi cha pili, Zambia walianza kwa kurekebisha kikosi chao, kocha Mfaransa, Herve Renard akiwatoa Hichani Himonde, Moses Phiri, Sinkala na Isaac Chansa na nafasi zao  kuchukuliwa na Stopila Sunzu, Mukuka Mulenga, Evans Kangwa na Francis Kasonde.

Pamoja na mabadiliko hayo, Stars iliendelea kung’ara na katika dakika ya 57 Ngassa alikaribia kufunga tena kama si shuti lake kufuatia pasi ‘tamu sana’ ya Sure Boy kutoka nje.

Lakini kukosa kwa Ngassa bao hilo, kulitokana na maarifa ya beki wa TP Mazembe ya DRC, Stopila Sunzu anayejiandaa kuhamia Reading ya England, ambaye alimbana kiungo huyo wa Simba kumynima mwanya wa kupiga vizuri na akafanikiwa kumfanya apige nje.

Zambia walipoteza nafasi nzuri ya kusawazisha bao dakika ya 76, baada ya shuti la Chasamba Lungu kugonga mwamba, wakati kipa Juma Kaseja akiwa amekwishapotea maboya.

Ngassa alijibu shambulizi hilo dakika ya 77 baada ya shuti alilojaribu kupaa juu ya lango, huku Felix Katongo akipewa kadi ya njano, baada ya kumuangusha Amri Kiemba aliyekuwa anamfunga tela.

Juma Kaseja alifanya kazi ya ziada dakika ya 86, baada ya kuokoa shuti la karibu la Chris Katongo na katika dakika ya 87, Stars ilipata pigo baada ya beki Kevin Yondan kuumia na nafasi yake kuchukuliwa beki mwenzake wa Yanga, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ dakika ya 88.

Kikosi cha Stars leo kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kevin Yondan/Nadir Haroub dk 87, Frank Domayo, Salum Abubakar, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Mrisho Ngassa/Amir Maftah dk83 na Khamis Mcha ‘Vialli’/Simon Msuva dk59.

Zambia; Danny Munyao, Chintu Kampamba, Hichani Himonde, Chisamba Lungu, James Chamanga, Moses Phiri, Chris Katongo, Felix Katongom Nathan Sinkala/, Rodrick Kabwe na Isaac Chansa. 

 

 

AZAM FC imefanikiwa kuingia Nusu Fainali ya Kombe la Hisa
ni mjini hapa, baada ya kuilaza Real de Kinshasa kwenye Uwanja wa Martyrs, katika mchezo maalum wa kutafuta timu ya kutinga Nusu ya michuano hiyo inayoandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka DRC.
Shukrani kwao, washambuliaji Gaudence Mwaikimba na Seif Abdallah waliofunga mabao hayo, moja kila kipindi.
Ikiongezewa nguvu na nyota wake watatu, Kipre Tchetche, Kipre Balou raia wa Ivory Coast na Mkenya, Joackins Atudo waliochelewa mechi mbili za awali, Azam leo ilitawala mchezo na kama si rafu za wapinzani wao, ingevuna ushindi mtamu.
Hadi mapumziko, tayari Azam walikuwa mbele kwa bao 1-0
, lililotiwa kimiani na Mwaikimba dakika ya 21, ambaye aliunganisha pasi nzuri ya Kipre kutoka wingi ya kushoto.
Hilo linakuwa bao la pili kwa Mwaikimba, mshambuliaji wa zamani wa Kahama United, Ashanti United, Yanga, Prisons na Kagera Sugar katika mechi tatu za mashindano haya alizocheza, awali alifunga katika sare ya 1-1 na Dragons.
Kipre Tchetche alilazimika kutoka nje ya Uwanja dakika ya 43 kutokana na rafu za wachezaji wa Real, nafasi yake ikichukuliwa na Samih Hajji Nuhu.
Real walikuwa wakipiga kiatu haswa na kiungo Waziri Salum aliungana na Kipre Tchetche kuuacha Uwanja kabla ya filimbi ya kuugawa mchezo, ingawa nafasi yake ilichukuliwa na Uhuru Suleiman dakika ya kwanza ya kipindi cha pili.
Awali ya hapo, refa Madila Achille alimtoa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 43 beki Muipalayi Igongo kwa kumchezea rafu mbaya Gaudence Mwaikimba, ambayo
 chupuchupu naye imtoe nje, kiasi cha kulazimika kumalizia mechi akichechemea.
Kipindi cha pili, Azam waliendelea kuwafundisha soka Real na katika dakika ya 73, kazi nzuri ya Mwaikimba ilisaidia kupatikana bao la pili. Mpira mrefu uliopigwa na kipa Mwadini Ally, Mwaikimba aliumiliki vema, akatoa pasi pembeni kushoto kwa Hajji Nuhu ambaye aliingia ndani kidogo na kukata krosi maridadi iliyounganishwa kimiani na Seif.
Humphrey Mieno alikuwa mwathirika mwingine wa rafu za Real, baada ya kulazimika kutoka nje dakika ya 77, akimpisha Abdi Kassim ‘Babbi’.
Azam walionekana kuridhika baada ya kuwa wanaongoza mabao 2-0 na wakafanya uzembe uliowapa bao la kufutia machozi Real, lililofungwa na Bisole Panzu dakika ya 78.
Baada ya mechi hiyo, kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall aliwapongeza vijana wake, lakini akasema anakabiliwa na wakati mgumu katika hatua inayofuata kutokana na wachezaji wake wanne kuumia leo.
Kocha wa Real, Sandra Makombele aliwasifu Azam ni timu nzuri na 
akasema anakubali matokeo, ingawa aliwapiga kijembe. “Wachezaji wangu wana mazoezi mengi, Azam hawana mazeozi, wakiguswa kidogo wanaumia, hakukuwa na rafu, ule ni mchezo wa nguvu kama Ulaya, kocha wao inabidi awape mazoezi mengi wawe wagumu,”alisema mwanamama huyo.
Katika mechi zake mbili za awali za Kundi B, Azam ilitoka 1-1 na Dragons na ikafungwa 2-0 na Shark FC.
Azam ilicheza mechi zote mbili bila makocha wake wote wawili, Waingereza Stewart Hall na Msaidizi wake, Kali Ongala ambao walibaki Nairobi, Kenya pamoja na Daktari Mjerumani Paulo Gomez na wachezaji Kipre Balou na Kipre Tcheche raia wa Ivor

 

y Coast, kutokana na kukosa viza za kuingia DRC.
Watano hao, waliwasili mjini Kinshasa jana na beki Joackins Atudo naye amewasili leo na wote wameshiriiki mchezo wa leo kikamilifu.
Nusu Fainali zitachezwa Desemba 25 wakati Desemba 26 itakuwa Fainali na mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Mwadini Ally, Himid Mao, Waziri Salum/Uhuru Suleiman dk46, Omar Mtaki/Joackins Atudo dk46, David Mwantika, Jabir Aziz, Kipre Balou/Malika Ndeule dk85, Seif Abdallah, Kipre Tchetche/Samih Hajji dk43, Humphrey Mieno/Abdi Kassim dk77 na Gaudence Mwaikimba.

 

YAW BERKO EDITED

SASA rasmi, Yaw Berko 
mebaki historia ndani ya klabu ya Yanga. Hiyo inafuatia klabu ya St Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuridhika naye baada ya majadribio.
Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameiambia fzakar.blogspot.com jana kwamba kipa huyo Mghana amefuzu majaribio Lupopo na amesajiliwa moja kwa moja.
Kuondoka kwa Berko, kunatoa nafasi kwa kiungo kutoka DRC, Kabange Twite kusajiliwa katika klabu hiyo ya Jangwani, akiungana na kaka yake, beki Mbuyu Twite. Wachezaji wengine wa kigeni wa Yanga ni kiungo Haruna Niyonzima kutoka Rwanda na washambuliaji Didier Kavumbangu kutoka Burundi na Hamisi Kiiza kutoka Uganda.
Berko alijiunga na Yanga SC mwaka 2009, akitokea Liberty Proffessional ya kwao Ghana, timu ambayo ilimuibua pia

 

 Michael Essein na nyota wengine kibao wa Ghana. Aliletwa nchini na kocha wa zamani wa Yanga, Mserbia Kostadin Bozidar Papic aliyewahi kupiga kazi Ghana katika klabu ya Hearts POf Oak.
Alikuwa kipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Bara msimu wa 2010/2011 na katika kipindi chake cha kufanya kazi Jangwani, anajivunia kuiwezesha timu kutwaa mataji ya ubingwa wa Bara msimu wa 2010/2011 na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mara mbili mfululizo, 2011 na 2012.
2011 alidaka mechi zote, lakini 2012 alidaka hadi Robo Fainali alipoumia na kumuachia Ally Mustafa ‘Barthez’ aliyedaka hadi ubingwa. Yanga imeridhika na uwezo wa Barthez langoni iliyemsajili kutoka Simba msimu huu na kuamua kuachana na Berko, ambaye alikuwa kipenzi cha wapenzi wa klabu hi

 

yo.
Awali, Yanga ilijifikiria mara mbili kuachana na Berko, kwa kuhofia Barthez angeanza ‘kuwaringia’ kwa kuona amebaki peke y
ake kipa bora, lakini imepanga kumhamasisha Said Mohamed kuimarisha kiwango chake, vinginevyo atatemwa mwishoni mwa msimu.
Na Yanga imekuwa na ‘jeuri’ ya kumtema Berko baada ya kuona mwakani haitashiriki michuano ya Afrika, zaidi ya Ligi Kuu na jukumu la kwenda kutetea taji lake la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame mjini Kigali, Rwanda.
Japokuwa anaondoka, lakini kwa uhodari wake langoni, Berko atabakia kwenye kumbukumbu ya mashabiki wa Yanga.
 
WASIFU WAKE:
JINA: Yaw Berko
KUZALIWA: Oktoba 13, 1980

 

ALIPOZALIWA: Accra, Ghana
KLABU ZA AWALI:
Mwaka Klabu
2000-2005: Liberty Professional
2005-2006: Pisico Binh Dịnh F.C. (Vietnam, mkopo)
2006-2009: Liberty Professional
2009- 2012: Yanga SC
2012: St Eloi Lupopo 

TIMU YA TANZANIA YA AZAM FC-FOOT BALL CLUB LEO IMEANZA NA SARE WAKIWA DRC-                          CONGO,WAKIFUNGANA 1-1.                            

              

TIMU YA TANZANIA YA AZAM FC-FOOT BALL CLUB LEO IMEANZA NA SARE WAKIWA DRC-CONGO,WAKIFUNGANA 1-1.

 

KOCHA wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 24 kitakachoingia kambini jioni ya Desemba 12 mwaka huu kuajianda kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia.

Katika kikosi hicho, wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Aishi Manula anachezea kikosi cha U20 cha Azam na timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), beki wa kushoto wa Azam, Samih Nuhu, beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid na mshambuliaji wa Azam, Mcha Khamis.

Pia kati ya wachezaji walioitwa, sita walikuwa kwenye kikosi cha Zanzibar (Zanzibar Heroes) kilichokamata nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi jijini Kamapala, Uganda. Wachezaji hao ni Mwadini Ally, Nassoro Masoud Cholo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Samih Nuhu, Aggrey Morris na Mcha Khamis.

Kikosi kamili kilichoitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally na Aishi Manula (Azam U20). Mabeki ni Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nassoro Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Samih Nuhu (Azam), Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Yanga), Amir Maftah (Simba), Issa Rashid (Mtibwa Sugar) na Kevin Yondani (Simba).

Viungo ni Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd Chuji (Yanga), Mrisho Ngasa (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Mcha Khamis (Azam), Salum Abubakar (Azam), Amri Kiemba (Simba) na Mbwana Samata (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- DRC).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC) na Mwinyi Kazimoto (Simba).