PICHA ZA SIMBA SPORT CLUB NA AZAM FC, LEO MECHI ILI KUWA NGUMU KIDOGO KWA AZAMFC  WAMEFUNGWA 3-1 ASAHIVI SIMBA SPORT CLUB IPO JUU SANA KWA POINT.NA YANGA SPORT CLUB WAMEFANIKIWA KUWA FUNGA JKT OLJORO BAO 1-0.

Advertisements

Mpira umemalizika, JKT Oljoro 0 – 1 Young Africans
Twite dkk 53

Dakika ya 87, Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Nurdin Bakari anatoka Frank Domayo
Dakika ya 79 Young Africans inafanya mabadiliko, anaingia Jeryson Tegete anatoka Didier Kavumbagu
Dakika ya 75, JKT Oljoro 0 – 1 Young Africans
Twite dkk 53

Dakika ya 60, JKT Oljoro 0 – 1 Young Africans
Dakika ya 53, Mbuyu Twite anaipatia Young Africans bao la kwanza

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza, JKT Oljoro 0 – 0 Young Africans

Mpira ni mapumziko, JKT Oljoro 0 – 0 Young Africans

Dakika ya 30, JKT Oljoro 0-0 Young Africans
Dakika ya 15, JKT Oljoro Vs Young Africans
Mpira umeanza hapa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kati ya
JKT Oljiro Vs Young Africans

Kikosi cha watoto wa Jangwani kinachoanza leo ambacho tumefanikiwa kukipata muda mfupi kabla ya mchezo kuanza.

1.Ally Mustapha ‘Barthez’
2.Shadrack Nsajigwa
3.Oscar Joshua
4.Nadir Haroub ‘Cannavaro’

5.Mbuyu Twite
6.Athuman Idd ‘Chuji’
7.Saimon Msuva
8.Frank Domayo
9.Didier Kavumbagu
10.Hamis Kiiza
11.Haruna Niyonzima

Susbs:
1.Yaw Berko
2.Nurdin Bakari
3.David Luhende
4.Kelvin Yondani
5.Rashid Gumbo
6.Nizar Khalfani
7.Jeryson Tegete

DK 90: mba 0 – 0 Mgambo DK 84: Okwi anapiga shuti kali linalogonga mwamba na kurudi uwanjani.

DK: 80: Muda unazidi kuyoyoma na Simba wanaendelea kulishambulia lango la Mgambo. Pia wanaongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji anatoka Ngasa anaingia Edo Christopher.

DK 70: Cholo anaingia vizuri mpaka kwenye sita ya Mgambo lakini anatoa krosi mbovu inayotoka nje.

DK 66: Issa Kinduru anapiga shuti kali katika lango la Simba na linatoka pembeni kidogo mwa goli.

DK 57: Simba wanaamka sasa, Amir Maftah anachezewa rafu nje kidogo ya eneo la hatari na Okwi anapiga faulo inayotoka nje kidogo ya lango la Mgambo.

DK 51: Simba 0 – 0 Mgambo

Kipindi cha pili kimeanza kati ya Simba na Mgambo JKT uwanja wa Mkwakwani.

HALF TIME

DK 43: Jonas Mkude anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa Mgambo.

DK 38: Mgambo wanalisakama sana lango la Simba lakini ukosefu wa umakini ndani ya 18 unawagharimu magoli.

DK 35: Milango bado migumu timu zote zinashambulianakwa zamu lakini wanashindwa kutumia vizuri nafasi wanazopata.

DK 28: Mgambo wanaingia kwenye lango la Simba na kufanya shambulizi kali lakini shuti linalopigwa na mchezaji Issa Kinduru linadakwa na Juma Kaseja.

DK 25: Kwa muda sasa Mrisho Ngassa amekuwa akiisumbua sana ngome ya Mgambo, anafanya shambulizi kali kwa ku[piga shuti linatoka nje kidogo ya lango la Mgambo.

DK 20: Simba 0 – 0 Mgambo

DK 15: Timu ya JKT Mgambo inaonekana kucheza vizuri zaidi ya Mnyama, wakijituma kufanya kila wanachoweza kuweza kupata bao la mapema.

DK 5: Simba 0 – 0 Mgambo

Mpira umeanza hapa uwanja wa Mkwakwani Mkoani Tanga.

VIKOSI VINAVYOANZA

SIMBA
1: Juma Kaseja

2: Said Nassoro Chollo
3: Amir Maftah
4: Hassan Hatibu
5: Pascal Ochieng
6: Jonas Mkude
7: Amri Kiemba
8: Mwinyi Kazimoto
9: Sunzu
10: Okwi
11: Mrisho Ngassa

MGAMBO

1: Gudson Mmasa
2: Yasin Awadhi
3: Salu Mlima
4: Bakary Msama
5: Salum Kipana
6: Ramadhan Malima
7: Chande Magoja
8: Musa Ngunda
9: Issa Kanduru
10: Fuly Maganga
11: Juma Mwinyimvua

KLABU ya Azam imeomba mechi zake za nyumbani dhidi ya Yanga na Simba zichezwe kwenye Uwanja wake wa Chamazi, maarufu kama Azam Complex ulioko Chamazi badala ya Uwanja wa Taifa.
Kuhusu maombi hayo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema yatawasilishwa kwenye kikao cha Kamati ya Ligi ya TFF kinachotarajiwa kufanyika leo mjini Dar es Salaam.
TFF iliamua mechi zote za Simba na Yanga dhidi ya timu za Dar es Salaam na Pwani, zichezwe kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa sababu ya idadi kubwa ya mashabiki wanaotarajiwa kuingia uwanjani, wakati viwanja vya Chamazi na Mabatini, Mlandizi unaotumiwa na Ruvu Shooting ni vidogo.
Awali, TFF ilipanga Ruvu Shooting na Yanga zicheze kwenye Uwanja wa Chamazi pia Oktoba 20, mwaka huu, lakini klabu hiyo inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kitengo cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), imeomba mechi hiyo ichezwe Uwanja wa Taifa.
Ingawa Ruvu Shooting haijasema sababu za kuomba mechi hiyo ichezwe Taifa badala ya Chamazi, lakini dhahiri wanataka kunufaika na mapato kutokana na ukubwa wa Uwanja wa Taifa.

BAO pekee la Themi Felix katika dakika ya 67, jioni ya leo limewapa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Felix aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mnigeria, Enyinna Darlington kwa kumtungua bao hilo, kipa Mghana wa Yanga, Yaw Berko, ameendeleza rekodi yake kuvifunga vigogo, Simba na Yanga katika Uwanja huo.

Hiyo inakuwa mechi ya pili Yanga kufungwa ndani ya mechi sita walizocheza hadi sasa na mbili wametoka sare- maana yake inabaki na pointi zake nane na kuzidi kujipunguzia matumaini ya ubingwa msimu huu, ikiwa sasa inazidiwa pointi nane na vinara wa ligi hiyo Simba SC.

Aidha, hii ni mechi ya pili Yanga inacheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi Ernie Blandts aliyerithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet na katika mechi hizo mbili ameambulia pointi moja kutokana na sare dhidi ya Simba Jumatano.

Kwa ujumla Yanga haijashinda hata mechi moja ya ugenini kati ya tatu ilizocheza hadi sasa, ilitoka 0-0 na Prisons, ikafungwa 3-0 na Mtibwa na leo imechapwa 1-0 na Kagera Sugar, wakati Alhamisi itacheza na Toto African mjini Mwanza.

Katika mechi hiyo, Yanga ilipata pigo dakika ya 23 baada ya mshambuliaji wake mahiri na tegemeo, Said Bahanuzi ‘Spider Man’ kuchanika nyama za paja dakika ya 23, baada ya kugongana na beki Benjamin Effe wa Kagera Sugar na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Jerry Tegete.

Tangu ajiunge na Yanga akitokea Mtibwa Sugar msimu huu, leo Bahanuzi amecheza mechi ya 13 kwa dakika hizo 23 na ameifungia timu hiyo jumla ya mabao 12, matatu kati ya hayo kwa penalti.

Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Omar Juma kutoka Mwanza, aliyesaidiwa na Dominick Nyamsana wa Dodoma na Hassan Zani wa Arusha, kikosi cha Yanga kilikuwa; Yaw Berko, Juma Abdul, Stefano Mwasyika/nurdin, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan, Frank Domayo, Didier Kavumbangu, Said Bahanuzi/Jerry Tegete na Haruna Niyonzima.

Kagera; Andrew Ntala, Jumanne Nade, Salum Kanoni, Amandus Nesta, Benjamin Effe, Malegsesi Mwangwa, Daudi Jumanne, George Kavilla, Enyinna Darlington/Themi Felix, Shijja Mkinna na Wilfred Emmeh/Paul Ngway.
Katika mechi zilizochezwa jana, Simba SC ilizidi kujiimarisha kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-1 ilioupata kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, ambayo ilimaliza pungufu ya wachezaji wawili baada ya kipa wake Shaibu Issa na mshambuliaji Meshack Nyambele kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.

Katika mechi hiyo iliyochezeshwa na refa Amon Paul wa Mara, aliyesaidiwa na Anold Bugabo wa Singida na Charles Simon wa Dodoma, hadi mapumziko Simba walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-1, mabao yake yote yakitiwa kimiani na kiungo Amri Ramadhan Kiemba katika dakika za 16 na 44, wakati la Oljoro lilifungwa na Paul Nonga dakika ya 29.

Kiemba alifunga bao la kwanza akiunganisha krosi pasi ya Christopher Edward, wakati bao la pili lilitokana na krosi ya Nassor Masoud ‘Chollo’, yote kutokana na mashambulizi ya upande wa kulia.

Ilikuwa rahisi kwa Kiemba kufunga mabao yote akiwa kwenye eneo la hatari, kutokana na mabeki wa Oljoro kumuwekea ulinzi zaidi Felix Sunzu.

Nonga naye alifunga bao lake baada ya kupewa pasi ndefu na kumpiga chenga kipa na Nahodha wa Simba, Juma Kaseja upande wa kulia mwa Uwanja na kuutumbukiza mpira nyavuni kiulaini.

Bao hilo lilitokana na beki Paul Ngalema kupokonywa mpira wakati amepanda kusaidia mashambulizi na Oljoro wakafanya shambulizi la haraka.

Kipindi cha pili Simba walirudi vizuri zaidi uwanjani na kuuteka zaidi mchezo- jambo ambalo liliwafanya Oljoro wawapunguze kasi kwa kuwachezea rafu. Hilo liliwagharimu kupoteza wachezaji wao wawili kabla ya filimbi ya mwisho na kufungwa mabao mawili zaidi.

Dakika ya 83 Mganda Emanuel Okwi aliifungia Simba bao la tatu na katika dakika ya tatu ya muda wa nyongeza baada ya kutimu dakika 90 za mchezo, Okwi akiwa anaelekea kufunga tena, alikwatuliwa na kipa wa Oljoro Shaibu Issa na refa akaamuru penalti sambamba na kumtoa nje kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja mlinda mlango huyo.

Awali ya hapo, Oljoro ilimpoteza mchezaji mwingine, Nyambele dakika ya 78, ambaye alionyeshwa njano ya pili kwa rafu aliyomchezea Jonas Mkude. Nahodha Kaseja alitaka kwenda kupiga, lakini akazuiwa na Felix Mumba Sunzu akaenda kufunga bao la nne kwa mkwaju wa penalti.

Kwa ushindi huo, Simba imefikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, hivyo kuendelea kuongoza Ligi Kuu, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 13, ingawa imecheza mechi tano.

Katika mechi nyingine za jana, Mgambo imepata ushindi wake wa kwanza baada ya kuichapa Polisi Morogoro 1-0, wakati Toto African imeichapa JKT Ruvu 2-1 na Prisons imelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar.

SIMBA SC imezidi kujiimarisha kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia  ushindi wa mabao 4-1 ilioupata jioni ya leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha, ambayo ilimaliza pungufu ya wachezaji wawili baada ya kipa wake Shaibu Issa na mshambuliaji Meshack Nyambele kutolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili.

Tiketi kwa ajili ya mechi ya Yanga na Simba itakayochezwa keshokutwa (Oktoba 3 mwaka huu) zitaanza kuuzwa kesho (Oktoba 2 mwaka huu) kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Mechi hiyo namba 80 ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara itachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 1 kamili usiku.

Vituo vitakavyotumia kuuza tiketi hizo kuanzia saa 4 asubuhi ni Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Uwanja wa Taifa, Kituo cha Mafuta OilCom Ubungo, Mgahawa wa Steers ulioko Mtaa wa Ohio/Samora, Dar Live Mbagala na Kituo cha Mafuta Buguruni.

Kiingilio cha chini kwenye mechi hiyo ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani ambavyo ni 19,648 kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 60,000. Watazamaji watakaoketi kwenye viti vya rangi ya bluu ambavyo ni 17,045 watalipa sh. 7,000 kwa tiketi moja.

Sh. 10,000 ni kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 wakati VIP C inayochukua watazamaji 4,060 itakuwa sh. 15,000. Kwa upande wa VIP B tiketi ni sh. 20,000 na VIP A yenye watazamaji 748 tu kiingilio kitakuwa sh. 30,000.