YANGA YAIFUNGA AFRICAN LYON 3-1

                                                             kikosi cha  AFRICAN LYON.
                                         KIKOSI CHA YOUNG AFRICAN-TANZANIA.
                                        TIMU ZIKI INGIA KUANZA MCHEZO LEO-DAR-ES-SALAAM.
                                                       WAKISALIMIANA WA CHEZAJI.
                                                KAVUMBAGU AMEACHIA SHOOT KALI LA MBELE.
                     MASHABIKI WA YOUNG AFRICAN WAKIFUNIKA UWANJANI-DA-ES-SALAAM.
                             MCHEZAJI WA YOUNG AFRICAN AKIJARIBU KUMTOKA MWENZAKE.
                          MCHEZAJI WA YOUNG AFRICAN AKIWATOKA WACHEZAJI WA AFRICAN LYON.
                                                MASHABIKI WA AFRICAN LYON.
           KAVUMBAGU  ANACHIA SHOOT  KALI KATIKA  HATARINI MWA AFRICAN LYON.
                                       MCHEZAJI WAAFRICAN LYON AKIMTOKA YOUNG AFRICAN.

YANGA SPORT CLUB LEO IME IBUKA NA USHINDI WA MABAO 3-1KATIKA UWANJA WATAIFA DAR-ES-SALAAM MAGOLI HAYO YALIFUNGWA NA NIZAR KHALFAN NA  NADIR HAROUB CANNAVARO

Advertisements

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom

Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya pili kesho (Septemba 19, 2012) kwa timu zote 14 kuumana katika viwanja saba tofauti nchini.
Wakati Simba ikiwa mgeni wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Yanga kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.
Viingilio kwa mechi ya Uwanja wa Taifa vitakuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 wakati kwenye Uwanja wa Jamhuri itakuwa sh. 3,000 kwa sh. 10,000.
Mechi nyingine za ligi hiyo zitakazochezwa kesho ni African Lyon vs Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. Nayo Ruvu Shooting itashuka kwenye Uwanja  wake wa Mabatini, Mlandizi kuikabili Mgambo Shooting kutoka Handeni mkoani Tanga.

Tanzania Prisons itakuwa kwenye Uwanja wake wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya kuisubiri Coastal Union ya Tanga wakati Oljoro JKT itaitembelea Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza utashuhudia mechi kati ya wenyeji Toto Africans na Azam.

Siku ya jumamosi tarehe 15, mwezi wa tisa mwaka 2012, soka la Tanzania lilitengeneza historia nyingine mbaya.

Ilikuwa ni siku ya ufunguzi wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara na timu mbalimbali zilikuwa viwanjani kutupa karata zao za mwanzo kabisa ndani ya msimu mpya wa 2012/13. Miongoni mwa mechi zilizokuwa zichezwe siku hiyo ilikuwa ni mechi kati mabingwa watetezi Simba na African Lyon zote kutoka Jijini Dar es Salaam.

Mapema asubuhi ya siku hiyo kulikuwa na mkutano wa waaandishi wa habari ulioitishwa na African Lyon na kampuni ya mawasiliano ya  simu za mkononi ya Zantel ambao siku hiyo walikuwa wameamua kutangaza rasmi muunganiko wao wa kibiashara – ambapo klabu hiyo itakuwa ikidhaminiwa na Zantel kwa muda wa miaka mitatu.

Hii ilikuwa habari nzuri kwa wapenda maendeleo ya soka wa Tanzania ikizingatiwa ni vilabu vichache tu ndivyo ambavyo vilikuwa vina udhamini hivyo kuwa na nguvu kuliko vilabu vingine na mwisho wa siku ushindani wenye tija katika kuukuza mpira ukawa sio mkubwa. Hivyo kuingia kwa Zantel kuidhamini African Lyon kulimaanisha kutaipa nguvu klabu hiyo kuweza kupambana na vilabu vingine vyenye fedha na nguvu kama Simba, Yanga, Azam, Mtibwa na nyinginezo.

Muda ukapita na saa ya kwenda uwanjani ikafika, timu zote zikawasili uwanjani na kuanza maandalizi ya mchezo. Kama ilivyo ada, kutokana udhamini ulivyo Simba ambao udhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro walikuwa na jezi zao zenye nembo ya mdhamini wao na wakaenda kuweka mabango yao ya mdhamini wao pembeni mwa uwanja – African Lyon nao baada ya kuwa wameshakamilisha udhamini wa Zantel, walikuwa na jezi zao zenye nembo ya mdhamini wao na pia wakaenda kuweka mabango uwanjani kama ilivyokuwa kwa Simba. Lakini cha ajabu ikatolewa amri kutoka TFF kwamba African Lyon hawatoruhusiwa kuvaa jezi za mdhamini wao mpya na mabango yao yakatolewa dimbani – huku sababu ikitoka kwamba hairuhusiwi kwa timu binafsi inayoshiriki ligi kuu kuwa na udhamini wa kampuni ya simu tofauti na Vodacom ambao ndio wadhamini wakuu wa ligi kuu. Kwa maana hiyo African Lyon iliwabidi watafute jezi nyingine zisizo na nembo ya mdhamini wao mpya na mabango yao yote yakatolewa ndani ya uwanja wa taifa.

Kitendo kile hakikuwa kizuri na kilitishia hata mechi kuvunjika kwa sababu viongozi wa  African Lyon wanasema walifanya kila kitu kwa kufuta sheria na kanuni hivyo walikuwa sahihi, na walisisitiza hata katika kikao cha kabla ya mechi walipeleka jezi zao na zikapitishwa na kwa ajili ya kuchezewa katika mechi ya baadae.

Kiukweli kitendo kile ambacho kilikosa majibu ya kueleweka hakikuwa kizuri na kileleta aibu katika soka letu, pia kinaweza  kuwakimbiza wadhamini wengine ambao walikuwa na interest ya kuja kuwekeza kwenye soka letu.

BAADA YA MECHI
Kutokana na kitendo kile nilijaribu kufuatiliwa na kutaka kujua kiundani kwanini imekuwa tatizo kwa African Lyon kuwa na mdhamini ambaye ni mshindani wa kibiashara na mdhamini mkuu wa ligi.

Katika kufuatiliwa kwangu nimekuja kupata taarifa za kuaminika kutoka baadhi ya viongozi wakuu wa vilabu vya ligi kuu kwamba mpaka sasa hakuna mkataba wowote halali wa kibiashara baina ya vilabu hivyo na kampuni yoyote juu ya udhamini wa ligi kuu ya Tanzania bara ambayo msimu huu ipo chini ya vilabu kupitia kamati ya ligi. Kwa maana katibu mkuu wa TFF Bwana Angetile Osiah amekuwa akitoa taarifa za uongo juu ya udhamini mpya wa Vodacom kwenye ligi kuu.

Ni kweli kwamba kumekuwepo au kulikuwepo na mazungumzo ya kati ya Vodacom na vilabu kupitia mwakilishi wao TFF, lakini mpaka sasa hakuna mkataba wa kisheria ulio halali baina ya pande mbili kwa maana hiyo ligi haina mdhamini rasmi. Hivyo taarifa anazotoa katibu mkuu wa TFF sio sahihi.

Mkataba huo sio halali kwa kuwa hakuna kiongozi wa timu yoyote aliyesaini mkataba huo wa udhamini na Vodacom. Ukweli ni kwamba TFF kupitia Angetile Osiah alikuwa kama mdhamini(Guarantor) katika majadiliano na utiaji saini wa mkataba, hivyo ilipaswa kwanza viongozi wa vilabu kupitia viongozi wao Mzee Said Mohamed na Wallace Karia wasaini kwanza ndio wampe Guarantor wao TFF aweke saini, lakini haikuwa hivyo na kwasababu wazijuazo wenyewe Angetile Osiah akatia saini kwenye mkataba kabla ya vilabu kufanya hivyo.

Je kwa sababu zipi, mdhamini wa kwenye mkataba akawa na haraka ya kuusaini mkataba kuliko wahusika halisi kabisa ambao ni vilabu au kuna 10% ya kuhakikisha dili la udhamini linaenda pale anapopataka? Majibu anayo mwenyewe.

KWANINI VILABU HAVIJASAINI MKATABA MPYA NA MDHAMINI WA LIGI?
Viongozi wakuu wa vilabu wanasema sababu kuu walizoshindwana mpaka sasa na mdhamini wa ligi aliyepita ni tatu tu.

1: Mdhamini kutaka apate upekee – yaani asiyewepo mpinzani wa moja kwa moja wa kibiashara katika issue nzima ya kutoa udhamini katika ligi, kwa shirikisho na vilabu pia. Vilabu vikatoa kauli ya pamoja kwamba ili mdhamini mkuu aweze kupata haki ya upekee inabidi a-double fedha anayota kwa  mwaka, jambo ambalo Vodacom walilikataa.

2: Fedha za udhamini: Kwa mujibu wa viongozi wa vilabu ni kwamba mdhamini wa ligi aliyepita alitoa ofa ya kutoa kiasi cha Billioni 1.6 kwa kila mwaka ndani ya kipindi cha miaka 3, lakini viongozi wa vilabu wakalipinga hilo kwa kutoa sababu kwamba lazima kiwepo kipengele cha ongezeko la thamaini ya fedha – kwa maana shilingi billioni ya mwaka huu haitakuwa sawa na thamani ya mwaka au miaka miwili mbele. Kwa maana hiyo wakaomba liwepo ongezeko la asilimia 10 ya fedha wanayopewa kwa kila mwaka.

3: Pendekezo la tatu ni kwamba mkataba uwe wa miaka miwili na si mitatu. Suala hili pia  likakataliwa.

Mapendekezo haya matatu ndio yaliyochangia uchelewashaji au kutokuwepo kwa mkataba wa udhamini wa ligi ulio halali kisheria.

NINI KINAFUATA
Kwa taarifa nilinazo ni kwamba viongozi wa timu za ligi kuu walikuatana jana jioni jijini Dar Es Salaam ili kujadili namna ya kuepukana na ukiritimba wa TFF na mikataba yao, na ikiwa kutatokea kampuni yoyote yenye  kutaka kuidhamini ligi kuu lazima suala ya ‘exclusivity ‘ lisiwepo ama kuongeza kiasi cha pesa na kufikia walau shilingi za kitanzania bilioni tatu ili kuondoa aibu ambayo iliikumba soka ya Tanzania jumamosi.

Pia wakaafikiana kwamba ligi ya mwaka huu itaitwa “Ligi kuu ya Tanzania Bara” na sio vinginevyo, huku wakitoa kauli rasmi kwamba hawautambui mkataba wa udhamini na Vodacom kwa sababu sio halali kwa maana hakuna kiongozi yoyote wa klabu aliyetia saini mkataba huo.

Pia viongozi wa vilabu kwa pamoja wamesikitishwa sana na kitendo ilichofanyiwa African Lyon na kukilaani vikali.

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 67,793,000.

 

Washabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.

 

Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh. 3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.

 

Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.

 

Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 50,435,000.

 

112 WASHUHUDIA MECHI YA JKT RUVU v RUVU SHOOTING

Watazamaji 112 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting iliyofanyika jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

 

Mapato yaliyopatikana katika mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 3,000 na sh. 10,000 ni 340,000. Mgawo ulikuwa kama ifuatavyo; kila timu sh. 29,465.87, asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 51,864.40, maandalizi ya uwanja sh. 100,000 na tiketi sh. 89,916.

 

Kamati ya Ligi sh. 9,821.95, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,893.17, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 3,928.78, gharama za mchezo sh. 9,821.95 na uwanja sh. 9,821.95.

Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys)


Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inaendelea vizuri na kambi ya mazoezi katika mikoa ya Mbeya na Njombe ambapo leo jioni (Septemba 16 mwaka huu) itacheza mechi ya kirafiki mjini Makambako na timu ya Manispaa.

Serengeti Boys ambayo iko chini ya Kocha Jakob Michelsen na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo imeshacheza mechi nne mkoani Mbeya. Imecheza mechi hizo dhidi ya Tanzania Prisons, Mbozi United, Mbeya City na Kombaini ya Kyela na kupoteza moja tu.

Baada ya mechi ya leo, kesho (Septemba 17 mwaka huu) itacheza mechi ya mwisho mkoani Njombe dhidi ya Kombaini ya Makambako na kurejea Dar es Salaam siku inayofuata kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kabla ya mechi dhidi ya Misri.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika Machi mwakani nchini Morocco itachezwa Oktoba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MECHI YA SIMBA, LYON YAINGIZA MIL 67/-

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 67,793,000.

Washabiki 11,505 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambapo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Kila timu ilipata sh. 14,603,263.47 wakati asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyokatwa ni sh. 10,341,305.08.

Mgawo mwingine umekwenda kwa msimamizi wa kituo sh. 20,000, posho ya kamishna wa mechi sh. 114,000, mwamuzi wa akiba sh. 70,000, et iti.sh. 3,175,000, vishina kwenye tiketi (attachments) sh. 345,150, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.

Umeme sh. 300,000, ulinzi na usafi uwanjani sh. 2,350,000, Kamati ya Ligi sh. 4,867,754.49, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,920,652.69, uwanja sh. 4,867,754.49, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,947,101.86, gharama za mchezo sh. 4,867,754.49.

Nayo mechi ya ligi hiyo kati ya Tanzania Prisons na Yanga iliyochezwa jana (Septemba 15 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza sh. 50,435,000.

NA fzakar.blog

                                                           Kikosi cha simba sport club:
                                                                Kikosi cha Afican lyon
                        Emmanuel Okwi akiwatoka hapa wachezaji wa African lyon:
                                         Akuffor akishangilia goli lake la kwanza:
                                                 Emmanuel okwi akishangilia goli lake la Pili:
                               Mrisho khalfan ngasa akifunga goli lake la Tatu:
Nassor Masoud ‘Chollo’ anatia krosi
                                                chollo anamtupia krosi nassoro massoud:

SIMBA SC imeanza vema kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, jioni hii baada ya kuichapa mabao 3-0 African Lyon katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimiani na Emanuel Okwi dakika ya 33 baada ya kuwatoka mabeki wa Lyon na Nassor Masoud ‘Chollo’ dakika ya 36 akiunganisha krosi ya Mrisho Ngassa.

Lyon walikosa penalti dakika ya 35, baada ya mkwaju wa Sunday Bakari kupanguliwa na Juma Kaseja, kufuatia Mwinyi Kazimoto kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Kipindi cha pili, Lyon kidogo walirekebisha makosa yao, lakini bado Simba iliendelea kutawala mchezo na dakika ya 56, Danniel Akuffor aliifungia timu yake bao la kuhitimisha ushindi kwa mkwaju wa penalti, baada ya Emmanuel Okwi kuangushwa kwenye eneo la hatari.

Lilikuwa ni goli ya tano kwa Akuffor katika mechi sita tangu alipojiunga na Wekundu wa Msimbazi akitokea Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Alifunga goli moja wakati Simba walipoibwaga JKT Oljoro 2-1, akafunga pia moja katika ushindi 2-1 dhidi ya Mathare United na jingine moja katika sare ya 1-1 dhidi ya Sony Sugar ya Kenya katika mechi tatu za kirafiki zilizopigwa mjini Arusha.

Katika mechi ya nne ya kirafiki ambayo Simba  walilala 3-0 dhidi ya AFC Leopards ya Kenya, Akuffor alizimia uwanjani na kutolewa katika dakika ya 40 akiwa hajafunga, lakini alirejea kucheka na nyavu dhidi ya Azam FC katika mechi ya Ngao ya Jamii ambayo Simba walishinda 3-2, yeye akifunga moja kwa njia ya penalti kabla ya leo kukamilisha bao lake la tano katika mechi sita.

Simba SC; Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Amir Maftah, Shomary Kapombe, Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba, Haruna Moshi ‘Boban’, Daniel Akuffo/Ramadhan Chombo, Mrisho Ngassa/Abdallah Juma na Emanuel Okwi.

African Lyon; Abdul Seif, Johanes Kajuna, Hamadi Manzi, Sunday Bakari, Benedictor Mwamlangala, Sunday Hinju, Obina Salamusasa, Semmy Kessy, Iddi Mbaga, Jacob massawe na Yussuf Mlipili.

Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Yanga imelazimishwa sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Hamisi Kiiza, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Nizar Khalfan/Athumani Iddi, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Didier Kavumbangu/Simon Msuva na Stefano Mwasyika.

Kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, bao pekee la Abdulhalim Humud liliipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Kagera Sugar.

Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Abdulhalim Humud, Ibrahim Mwaipopo,  Himid Mao/Jabir Aziz, John Bocco, Abdi Kassim/Kipre Balou na Kipre Herman Tchetche.

Kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, bao pekee la kiungo Mkenya, Jerry Santo dakika ya 41 liliipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya Mgambo FC.

Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wenyeji Polisi wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar ya Turiani, Manungu.

Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, Toto Africans imelazimishwa sare ya 1-1 na JKT Oljoro, wakati Uwanja wa Chamazi, Mbagala, JKT Ruvu imeifunga Ruvu Shooting mabao 2-1.

MATOKEO MECHI ZOTE LIGI KUU LEO
Simba 3-0 African Lyon
Kagera Sugar 0-1 Azam FC
Prisons 0-0 Yanga
Coastal Union 1-0 Mgambo JKT
Toto African 1-1 JKT Oljoro
Polisi Moro 0-0 Mtibwa Sugar
JKT Ruvu 2-1 Ruvu Shooting