Timu za tanzania bara  zinazo julikana kama simba sport club b imeingia fainali…

 

Advertisements

Mrisho Khalfan Ngasa akitambulishwa rasmi katika kikosi cha Simba sport club leo.

kama unavyo ona  kundi la watu wakija kumunangalia

           hapa akifanya mazoezi ndani ya coco beach.
                                  hapa tena mazoezini
                   hapa akiongea na rafiki yake.
                  hapa akiwangalia wachezaji watimu yake.
       kundi la watu wanamshangilia kuja simba sport club.
   hapa meneja wakimtambulisha kwanza mrisho khalfan ngasa.
           mashabiki wa simba sport club wakionesha bango..

TIMU za Simba na ya Yanga zimekubali kushiriki mashindano ya Super 8 yanayodhaminiwa na Benki ya ABC

Thursday, August 2, 2012

TIMU za Simba na ya Yanga zimekubali kushiriki mashindano ya Super 8 yanayodhaminiwa na Benki ya ABC

TIMU za Simba na ya Yanga zimekubali kushiriki mashindano ya Super 8 yanayodhaminiwa na Benki ya ABC yatakayoshirikisha timu nane kutoka Tanzania Bara na Visiwani baada ya juzi kufikia makubaliano na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Hivi karibuni viongozi wa timu hizo walisikika wakisema kuwa timu zao hazitashiriki mashindano hayo kwa kile walichodai kuwa hayatawanufaisha ila TFF ndiyo itakayonufaika zaidi.
Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa viongozi wa timu hizo walifikia makubaliano hayo ya kushiriki katika mkutano uliofanyika juzi makao makuu ya shirikisho hilo.
“Tumefikia makubaliano na timu hizo, lakini pia kuna mambo ambayo walipendekeza yafanyiwe kazi na hivi sasa TFF inayafanyia kazi,” alisema Wambura.Katika hatua nyingine Wambura alisema kuwa mashindano hayo yanazinduliwa rasmi leo jini Dar es Salaam na yataanza Agosti 8 mwaka huu.
Mashindino hayo yatapigwa katika vituo vinne tofauti ambavyo ni Dar es Salaam, Arusha, Mwanza pamoja na Zanzibar, ambapo timu za Simba, Yanga, Azam, Polisi Morogoro zitashiriki kwa upande wa Tanzania bara.